Yutong na Scania

Yutong na Scania

sasa mbona matajiri hao hao wa mascania mbona wanaoleta yutong saizi. Sawa scania inadumu lkn ili upate faida inabidi ukae nayo miaka 6 wkt yutong miaka 2 tu imeleta faida. Kumbuka biashara ni faida
wewe unaangalia body tuu,yutong nyingi zimefungwa injini za scania ,gearbox na diff
 
Daaah kwa speed yutong ni mwisho mfano safari ya Dar-Mwanza,,,,mi huwa napoa sana maeneo ya natta,karibia kila siku zile yutong za super sammi ndo zinaongoza,,,kuna majamaa huwa wanasema hiyo gari ni zaidi ya dushelele,,,,,,,
Mkuu Dar Mwanza au Dar Kahama kwa mbio zinatisha Kisbo na Cityboy ambazo ni scania. Wakuu, scania ni namba nyingine ikishachanganya hakuna basi inayogusa. Uliza kuna happynation zilikuwa scania za mbeya hakuna basi ilikuwa inagusa. Scania busses zipo vzuri sana kwa mbio na uimara. Udhaifu pekee wa scania busses zilizokuwa zinakuja tz zilikuwa hazina AC. Ila hapa juzi kati nilipanda scania bus yenye ac ilikuwa matata sana.

Tukija kwa Youtong zinachakaa haraka sana; ukiangalia scania za abood hadi leo zipo fresh na zina kama miaka kama kumi hivi lkn yutong za BM zina miaka kama sita hivi lkn zmechoka mbaya.
 
mi atakaye niambia bus za mgamba barabara ya arusha-mwz kama ni yutong au scania ndo ntajua kati ya hzo yupi ni mkali
Unazungumzia Mghamba ipi, Sauti ya kamanda, pata kitu cha Arusha, au Misisipi? zile mashine ni Scania OG.
 
Mkuu Dar Mwanza au Dar Kahama kwa mbio zinatisha Kisbo na Cityboy ambazo ni scania. Wakuu, scania ni namba nyingine ikishachanganya hakuna basi inayogusa. Uliza kuna happynation zilikuwa scania za mbeya hakuna basi ilikuwa inagusa. Scania busses zipo vzuri sana.
Kuna ile Basi Scania ya Dar-Simiyu iliyopata ajali ikaua Abiria 48 ilikuwa inaitwa Simiyu Coach a.k.a Ndama Jeuri ile ilikuwa ni noma na ilikuwa inawakalisha magari yote ya hiyo njia ya Dar Shinyanga Mwanza. Ilikuwa inatoka Simiyu asubuhi inafika Dodoma mida ya saa6 mchana,na ilikuwa ikifika pale shughuli zote za stand zinasimama wapiga debe,wafanyabiashara na madereva wanaanza kuishangilia kwa kelele na miluzi.
 
Back
Top Bottom