Yutong/zongtong/Higer and scania buses

Wewe abiria anaanza kuangalia kwanza body is it attractive? On board products pia, Wachina wamekuwekea hadi usb port sasa unakuja na Marcopollo limeshachoka unafikir wabongo wako sensitive na time?
 
Samaritan nami nimekuelewa mchina anakuja kwa kasi sana na hii imesaidia kupunguza kupanda bei kwa mabasi mengine nami nimependa sana ujio wao ili kuondoa monopoly wa soko wa baadhi ya makampuni Afrika..
 
uzi mtamuu huu nitarudi baadae kutoa uzoefu wangu
 
Mwanapropaganda wanavyonunua wanaagiza body brazil ukiwa South Africa then unaenda Scania kununua chasis wao ndio wataunganisha kila kitu mara ya mwisho kwa walio na base Zambia wanadai ni usd 550,000 kwa kila kitu mimi naona ni ghari sana bora upate tuu yutong au used Scania matoleo ya sasa hivi..
 
Hivi mnayafahamu kisbo?
 
zainabs zilifungiwa baada ya kuuwa watu 52 pale luhimba mpakani mwa mkoa wa njombe na ruvuma kuna makaburi ya ukombusho pale toka afutwe na sumatra akavua bodi za basi na kubaki lori za mizigo na kwa kuwa alikua akifukuzana na shabiby wao wakafungiw ruti ya ruvuma
 

Ahsante kwa taarifa mkuu
 
kama swala la luxury ndugu yangu umeshapanda zile gari za modern cost ni scania ila ndani ni zaidi ya fast jet kuna zile za nairobi mombasa ni single siti kuna jamaa anaitwa air bus pale nairobi anachonga body wacha kabisa youtong zinasubiri
 
Scania ni gari nzuri sana kama mercedes actros tofauti kubwa iliyopo actros inatembea mazingira yote. Lami barabara ya vumbi na matope hata kukiwa hakuna njia yaani pori actros inapita. Scania shida yake ni kwenye matope huwa haina ujanja kabisa inaweza kukwama kirahisi kwenye tope. Actros haikwami labda ikalie dif zote mbili. Pamoja na hayo hakuna gari nzuri kwa barabara za africa kama scania na mercedes actros.
 
Gari za kichina zimekuja kwa wingi sana kwenye soko la Tanzania kwasababu ni cheap kwa bei na pia running cost lakini tatizo kubwa hazidumu. Zaidi ya asilimia 80 ya gari za kichina unazoziona ubungo zimefanyiwa overhaul zikiwa hata hazijamaliza miaka miwili. Halafu zina shida mojai kiua piston moja inabidi ubadili zote usipofanya hivyo baada ya safari zisizozidi kumi inaua piston zingine zote. Scania ukinunua mpya japo ghali sana unapewa guarantee ya 10yrs. Kama wewe ni mfuatiliaji angalia marcopolo za abood, hood, dar express, kilimanjaro utajua kuwazina zaidi ya miaka kumi na hazioneshi kama zimechoka.
 
Kaka
Wewe abiria anaanza kuangalia kwanza body is it attractive? On board products pia, Wachina wamekuwekea hadi usb port sasa unakuja na Marcopollo limeshachoka unafikir wabongo wako sensitive na time?
Nafikiri wewe ndio uko nyuma panda marcopolo mpya za dar express zinazoenda dar - nairobi utajua kama yutong ni cha mtoto. Hiyo basi ni 600m pale sub scania. Ni basi classic sana huwezi kujutia kuzipanda mwendo na nguvu sio vya kuuliza.
 
Kwa Tanzania(Africa?) hakuna mashine inaiweza scania
Mkuu nakuomba ingia Wikipedia, usiingie Google, utakuta option nyingi, ukiingia huko directly tafuta hizo Higer uone. Hao wachina ni kiboko. Tena wameingia ubia wa kitengo cha R&D,kimsingi walishirikiana kutoa Engine na hao Scania. So naamini Wachina wakiamua kutoa kitu kwa matumizi ya Wazungu kinakua cha ukweli mno
 
......Brother Hujawai Kupanda Scania Classic wew! Huzijui Scania Wew!! Nimepanda Classic Scania Nimepanda Classic Chinese Buses But Kumkuta Scania Hapana Badooooo!! Scania Labda Yupo Level moja na Kina Hyundai Sio Takataka Nyingne!! Kwanza Ubora wake Upo Juu Sana kuanzia Engine hadi seat Zake,Zina Seat Pana kam Ndege za Fly Emirates, Pili Zina Dumu Kwa Muda Mrefu sana Ukilinganisha na Hizi Bus zenu, Tatu Zinakimbia Sana Iwe Milimani, Tambarare au Mteremkoni
 
Ndo ujiulize na wewe ,wanaomiliki scania marcopolo new model ni wawili tuu tz nzima dar express na kaizirege tuu. Huo ni mziki mwingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…