Yutong/zongtong/Higer and scania buses

Yutong/zongtong/Higer and scania buses

Kaka situmii mchina. Ni kweli wachina wameshika soko kwa kigezo kimoja tu cha bei ya chini lakini ubora wa kazi zao ndio tatizo. Hata majengo.na barabara fuatilia kote wanakofanya kazi alafu baada ya miaka miwili uone hiyo barabara ilivyochakaa.

Kutokuwa na uwezo wa kifedha kunatupa shida sana katika kufanya maamuzi na huo ndio ukweli.
lakini mchina anakupa kitu kulingana na bajeti yako kaangalieni yutong zinazotumika huko ulaya
 
Kuna kipindi nilikuwa natumia sana usafiri wa ABOOD Scania toka Tunduma to Dar kipindi hicho ndo alikuwa anaongoza soko na zilikuwa zinatembea vizuri tu mara gafla akatoke mchina new force,Colour Star,Saibaba watu wote tukalikimbia ABOOD mpaka leo huwa anapakia abiria baada ya gari zote za mchina kuondoka sasa akaanza kujikosha maraa oohh siwezi nunua mchina sasa hivi nadhani ndo anaongoza kwa kuwa na gari nyingi za mchina hahahaahhaha hapana chezea mchina aiseeee anajua afanye nini na kwa wakati gani
Mkuu kama unakumbuka kulikua na newforce nyekundu ,vijifupi tulivibatiza jina new force vipisi , injin yake ipo nyuma.. Niliwah kukapanda mbeya-dar mbona nilitaman kushukia njian.. Dereve anaendesha kama ikitokea ajali jafi. N mwendo pitch kibati… anaovertk mpaka kitonga, yan anashuka kama haoni zile kona…
 
Tulieni Tanzania ya viwanda inakuja tutatengeneza mabasi yetu wenyewe
 
Kwa hio hata zile Mghamba zote, missisipi, amazon, captain, bughati, Suez canal, brigedia, sauti ya kamanda, air force one, Zambezi ni engine za malori?
Kuna hizo gari zenye engine ya scania Mghamba express kama sio traffic na mataa barabaran yaaan ni gari zinazowanyoosha madereva wote wa dar from Mwanza wanakuja kumkuta jamaa Singida kapoa lunch...nadhani mliowahi kupanda kipindi hcho mnazielewa hizi gar(Ndege za Arusha)
 
Ni bus ya shabibu iliyopata ajali mpakani kati ya njombe na songea kipindi hicho
 
tunaongelea injini hatuongelei mabody mkuu
hata mimi ninaongea habari ya injini ndio maana nimetoa hoja katka performance za gari ktk masafa marefu,milima na uimara wa gari kudumu muda mrefu. zile hood body zimechoka lakini injini zake ndo kwanza bado zinadai
 
hata mimi ninaongea habari ya injini ndio maana nimetoa hoja katka performance za gari ktk masafa marefu,milima na uimara wa gari kudumu muda mrefu. zile hood body zimechoka lakini injini zake ndo kwanza bado zinadai
[emoji28][emoji28][emoji28]Hood mashine kabadilisha mara ngapi pale
 
Mkuu kama unakumbuka kulikua na newforce nyekundu ,vijifupi tulivibatiza jina new force vipisi , injin yake ipo nyuma.. Niliwah kukapanda mbeya-dar mbona nilitaman kushukia njian.. Dereve anaendesha kama ikitokea ajali jafi. N mwendo pitch kibati… anaovertk mpaka kitonga, yan anashuka kama haoni zile kona…
Wanasema wanamwaga moto
 
Huyu haangalii market trends, kwa taarifa ni kuwa scania anaisoma namba habari ya mjini ni Yutong and the likes kwa mfano kampuni ulizotaja zinatumia scania yaangalie hayo mabasi yote yamezeeka, hebu taja basi moja tu jipya pale Ubungo model ya scania
Scania anaisoma namba kwenye soko lipi?
 
Mkuu miaka ya nyuma akikuepo dereva anaitwa Giriki na mwingine Cheupe ashawahi fika mbeya saa nane mchana imetoka Dar 12 alfajiri gari lilipiliza Central unazungumzia kipindi cha tochi na Sumatra mabasi yanatoka mbeya alfajiri na usiku...
kaka umenikbusha kuna jamaa alikua anaitwa msomari alikua akiendesha zainabs za songea alishawai fika songea sa kumi kasoro pale stendi watu wote walimshangilia sana zile kelele akazisikia RPC akaja kuuliza kulikoni wakamjibu wanamshangilia Msomari katoka dar palepale akatiwa sero
 
Mpepai huyu Giriki na mwingine Mwarabu walikua hatari sana kwa speed ila hawakuwa na rekodi ya ajali na ili basi liwe na abiria walikua wanachukuliwa kwa posho kubwa Giriki kakaa sana selo Iringa mpaka mara ya mwisho RTO aliapa ile njia hatopita alibadili ruti ya Dar Songea huko kukawa kwa moto ikabidi aende kwenye Maroli ya Mchanga alikua anakimbiza kitonga kama hakuna mlima wala kona kali...
 
Hapa Tanzania mchina ameshika soko japo sio kutokana na ubora ila bei ndogo ya basi zake. Hizi bus za higer kuna kitu nimekiona kwenye basi 3 nilizo safiri nazo njia ya dar tunduma (happy nation, dar lux, muro). Mfumo wake wa air suspension kujaza upepo kwenye booster za mbele haupo vizuri wakati gari haizijamaliza hata mwaka toka dukani. Basi zote 3 system zilikua zinapiga alarm njia nzima kwamba upepo haujai wa kutosha kwenye booster za mbele, happy nation pia alikua dereva alikua ana hangaika kuipata gia ya reverse mpaka akaamua ikienda dar ikarekebishwe.

Kwa basi mpya haitakiwi kuwa na majanga kama hayo kabisa na ina maanisha kuta upungufu katika utengenezaji wa hizo mashine.
 
cummins yenye 360hp kama hzi zhongtong inazidiwa na f310 sembuse f330 na kuendelea
 
mkuu hizo gari viaggio 1050G7 sidhani kama zinafika mil 900 kwa kipindi alichonunua dar express maana nilishawai kuuliza marcopolo sa wakasema hazipishani sana na bei ya Andare G6 vile vile kilimanjaro express yeye ananunua mabody kutoka marcopolo na kuyavisha chassis na injini za malori za mwanzo alifunga 94D hizi za sasa hivi kafunga P230 opticruise na upande wa gari za kichina ulishawai kuona yutonga f12,f9,Higer,goldendragon,kinglong,zhongtong climber imefungwa vitu vya scania??
Hiyo figure nimefanya exchange rate kutoka Dollar kwenda shilingi siku husika.KLM nilipata ukakasi baada ya kugundua body nizamacropolo hila ndani zipo used kuendana na muonekano wake ndani.
 
Hiyo figure nimefanya exchange rate kutoka Dollar kwenda shilingi siku husika.KLM nilipata ukakasi baada ya kugundua body nizamacropolo hila ndani zipo used kuendana na muonekano wake ndani.
kilimanjaro express body zile ni mpya kabisa wanachukulia marcopolo south africa chassis na injini ndio wanafunga za malori labda wewe ulipanda zile namba A kajaribu namba D
 
Back
Top Bottom