Yuwapi January Makamba wakati huu nchi ikiwa gizani?

Yuwapi January Makamba wakati huu nchi ikiwa gizani?

Teko Modise

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
2,331
Reaction score
7,733
Waziri wa Nishati, January Makamba yuwapi kwasasa? Sehemu kubwa ya nchi haina umeme mpaka mida hii. Waziri amekaa kimya?

Sawa najua TANESCO walitupa taarifa asubuhi, lakini kwa uzito wa suala hili Waziri alipaswa atoke hadharani atupe updates.

Yuwapi Januray Makamba?
 
Yupo bize na mradi wake wa nguzo imara za zege zisizokuwa na nondo ndani yake ambazo tayari mbili kwa taarifa rasmi zimeaha anguka
Sasa huoni kama zitakuwa bei poa zaidi ya zile nyingine 😂😂😂
 
Waziri ?!!! [emoji15][emoji15][emoji15]

Ulikuwa wapi kutoiona taarifa ya TANESCO?!!!

Wakati mwingine lawama hazitusaidii....[emoji1787][emoji1787]

Mtambo wa ubungo 2 uliharibika kusababisha gridi ya taifa zaidi ya megawati 200 kutokuwepo....

#SiempreJMT[emoji120]
Ndio umeandika utumbo gani?
 
Dp weldi imevuruga mambo sasa namna nzuri ya kuipoteza na kudhibiti mijadala inayondelea kwenye sosho media ngoja tuwape ugao wa umeme!!mawasiliano yawe hafifu hatutaki mpashane/na kuongeza habari za msingi kuhusu nchi!!
 
Moja ya project ya hovyo sana na gharama kubwa.

Yani ule ni ufisadi wa wazi kabisa ambao umebarikiwa na serikali.
Na nguzo zenyewe zinavunjika na kudondoka chini tena serikali ichukie tahadhari zisije leta madhara ya kuuwa watu zinapodondoka.
 
Ukatikaji wa umeme umeleta taharuki kubwa sana leo hospital ya KCMC na kuwapa taabu wagonjwa .

Taifa litakuwa limepata hasara kubwa mno naambiwa Leo jioni kwenye kivuko pale feri watu wameshindwa kutumia NCard kwa sababu mashine zilikuwa hazifanyi kazi kwa sababu ya kukosekana kwa umeme ikabidi raia wapite bure
 
Back
Top Bottom