Yuwapi January Makamba wakati huu nchi ikiwa gizani?

Yuwapi January Makamba wakati huu nchi ikiwa gizani?

Haya mambo ndio unayopata kwa kutegemea umeme wa serikali, Tanzania haina haja kabisa ya kuwa na tatizo la umeme, wape private corporations washindane wazalishe na kuuza umeme, serikali isimamie sera tuu na kuangalia kwa makini michezo michafu ya wafanyabiashara ili wasitupige, CCM haiwezi na haitoweza kuzalisha umeme wa kutosha, TANESCO ni kama fuko lao la kampeni na rushwa, kila wakiishiwa wanaenda kuchota, na bila umeme wa uhakika na bei nzuri sahau maendeleo
 
Si kweli...

Ona hili hapa....

Nchi 2 zinazoongoza kwa kuwa na umeme wa uhakika ni ICELAND na ISRAEL....kote huko serikali ndiyo inayohusika na kusimamia ,kuzalisha na kusambaza umeme....[emoji1787]

Marekani nako pamoja na private companies kuhusika ila FEDERAL GOVERNMENT inasimamia na kuzalisha sawia.....

Karibu Komoni hapa Sondombwa[emoji120]
US unaongelea less than 20% of government owned, TZ is like 100%, point ni TANESCO wamefeli na kwanini wanazuia private companies kufanya biashara ya umeme, ulitaka viwanda vya bia na simu viwe vya serikali navyo? what so special about electricity? hakuna haja ya kuzuia fursa ambayo itafanya watu wapate umeme na wapige hela kwa wakati mmoja
 
Waziri wa Nishati, January Makamba yuwapi kwasasa? Sehemu kubwa ya nchi haina umeme mpaka mida hii. Waziri amekaa kimya?

Sawa najua TANESCO walitupa taarifa asubuhi, lakini kwa uzito wa suala hili Waziri alipaswa atoke hadharani atupe updates.

Yuwapi Januray Makamba?
Anakula pipi nje ya nchi, pale kwake kuna majenereta ya kutosha hana mgao wowote
 
Waziri wa Nishati, January Makamba yuwapi kwasasa? Sehemu kubwa ya nchi haina umeme mpaka mida hii. Waziri amekaa kimya?

Sawa najua TANESCO walitupa taarifa asubuhi, lakini kwa uzito wa suala hili Waziri alipaswa atoke hadharani atupe updates.

Yuwapi Januray Makamba?
Waziri wa nini na TANESCO wameshatowa ufafanuzi? Soma Daily News ya leo, hata mtandaoni ipo.
 
Waziri wa nini na TANESCO wameshatowa ufafanuzi? Soma Daily News ya leo, hata mtandaoni ipo.
Hata mimi namshangaa eti anamuulizia waziri??
Waziri huyu aliyetamka watanzania kunamafuta kibao msidanganyike wakati watanzania wenyewe wanajionea kwa macho yao sheli pakavu. Hata mi nimemshangaa kumuulizia maana hachelei kusema umeme upo msidanganyike
 
Waziri wa Nishati, January Makamba yuwapi kwasasa? Sehemu kubwa ya nchi haina umeme mpaka mida hii. Waziri amekaa kimya?

Sawa najua TANESCO walitupa taarifa asubuhi, lakini kwa uzito wa suala hili Waziri alipaswa atoke hadharani atupe updates.

Yuwapi Januray Makamba?
January anajiandaa kuja kumtoa madarakani Mama Samia Suluhu Hasan hapo 2025.
 
Back
Top Bottom