Za ndaani kuhusu kocha ajaye Simba SC

Za ndaani kuhusu kocha ajaye Simba SC

za ndaani kabisaa wenyewee makolo wanasema kocha wao mpya wa msimu ujao yumo humu humu nchi kwa sasa anamalizana kimtindo na tim aliyo ipa ubigwaa then by next week anaibukia upande wao…………………….. sasa hii sijui ni ktk kukomoana, kwa kweli yajayo yanakera!
 

Imeeleza hadi kufikia jana, kulikuwa na makocha wawili ambao walikuwa wakiangaliwa kwa mara ya mwisho ili mmoja kupitishwa akiwemo kocha wa zamani wa RS Berkane ya Morocco raia wa nchi hiyo, Tarik Sektioui. Mwingine ni Jozef Vukušič raia wa Slovakia.

Taarifa ambazo imeripoti Gazeti la Spoti Xtra, zinasema kwamba, Sektioui ana nafasi kubwa ya kupewa mikoba hiyo.

Kocha huyo Oktoba 25, 2021, alikiongoza kikosi cha RS Berkane kutwaa Kombe la Shirikisho la CAF kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Pyramids FC ya Misri.

Chanzo chetu kutoka Simba, kimeweka wazi kwamba, baada ya uongozi kuchakata na kufanya mahojiano na makocha waliosalia kwenye ile orodha ya waliokuwa wakiwahitaji, Sektioui ameonekana kuwa na nafasi kubwa.

“Tayari tumeshapata kocha mkuu na kwamba taratibu zote za usajili unaoendelea kwetu, yeye ndiye ameshauri, ambapo miongoni mwa wachezaji waliokwishazungumza nasi, wawili atakuja nao mwenyewe pamoja na kocha wa viungo.

“Atakuja na kiungo mkabaji pamoja na straika mkali wa mabao, pia ametuelekeza kumsajili beki wa kati na winga ambaye yeye majina anayo,” kilisema chanzo hicho.

Kocha huyo Machi 7, 2021, alijiuzulu kuitumikia RS Berkane na nafasi yake ikachukuliwa na Kocha Juan Pedro Benali, raia wa Hispania, alipoondoka akateuliwa Florent Ibenge ambaye yupo hadi sasa.
Jamaa umeandika kwa upako mkubwa sana! 🙏
 
Kuna namna mbili za kumscout kocha, 1.based on performance/ ideas,
2.Based on CV, sijui timu zetu zinatumia ipi ila ya kwanza ni bora kuliko.
Kwangu nafikiri CV is not important lkn ni sehemu tu ya mafanikio
 
Viongozi waliopo Sasa wamekuja na mbio za mwenge mbaka mkija kukaa sawa mtakua mme Chakaaa.
Mbaka= mpaka.

Hivi mbona huwezi kuandika hili neno kwa usahihi au ni athari za lugha yako mama?
 
Hii ni list ya mchongo kabisa haiwezekani Nabi akosekane.

....... [emoji23][emoji23]Alisikika utopolo a,k,a chura mmoja akilia kutuka matopeni.....[emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hii ni list ya mchongo kabisa haiwezekani Nabi akosekane.

....... [emoji23][emoji23]Alisikika utopolo a,k,a chura mmoja akilia kutuka matopeni.....[emoji23][emoji23][emoji23]
Mlikuwa na kocha wa MADRID na haikuwa kesi, itakuwa huyo?.
 
Back
Top Bottom