Zaburi 113:7: Humwinua fukara kutoka mavumbini, humnyanyua maskini kutoka unyonge wake

Zaburi 113:7: Humwinua fukara kutoka mavumbini, humnyanyua maskini kutoka unyonge wake

Sasa lini? Mbona miaka inakatika sioni maajabu?
Huyo hiyo mali hajatafuta yeye, kaikuta tu! Walioitafuta hiyo ndio walipata shida kwa kupitia changamoto kama unazopitia wewe! Pengine ni babu wa babu yake! Hivyo na wewe fanyakazi kwa bidii ili kizazi chako kije kufurahia matunda yako!
 
Huyo hiyo mali hajatafuta yeye, kaikuta tu! Walioitafuta hiyo ndio walipata shida kwa kupitia changamoto kama unazopitia wewe! Pengine ni babu wa babu yake! Hivyo na wewe fanyakazi kwa bidii ili kizazi chako kije kufurahia matunda yako!
👏 👏 👏
 
Nimejifunza mambo haya katika maisha yangu, Mche Mungu wako, epuka kutenda dhambi, wapende watu wote pamoja na familia yako, toa msaada pale unapoweza, jaribu kuondoa uchungu kwenye moyo wako, wasamehe watu waliokukosea, jaribu kufurahi na kuwa na amani na watu wote na mwisho mwombe sana Mungu akusaidie kushinda vishawishi vya shetani maana ni vingi sana.
 
Acha uvivu, Fanya kazi, Tumia pesa kwa nidhamu, Jifunze kuwekeza mkuu!!

Mafanikio ni kuunganisha Codes tu, hayahitaji power from Source fulani.

Acha kujifunika na kujitetea kwa poroja za dini, Huyo Mungu angekua ana nia ya kuwainua wote muwe Matajiri asingeuumba Umasikini.

Kwanini kaumba umasikini wakati anataka wote muwe matajiri?
E mkuu umepiga pakubwa😀
 
Ufanye kazi sio utegemee zaburi. Hamchelewi kukalisha kombwe na kuzuia akili kuwaza kutatua changamoto za maisha mkisubiri zaburi itimie.
Ukafanye kazi sio usubiri muujiza wa kuinuliwa. HAta mtunga zaburi alifanya jitihada hakukalisha kombwe
 
Kwanza Mimi siyo aina ya mtu wa kutishika kuadhibiwa na kitu kisichothibitishika uwepo wake kwa kuzungumza ukweli kukihusu.

Eti kwamba nitapata matatizo kama nikimu-ignore huyo Yesu ambaye Infact ni Muongo.

Kama huyo yesu ataniadhibu sababu nina msema kwenye ukweli, Je yeye adhabu yake ya uongo ataadhibiwa na nani?

Maana alikufa Ijumaa saa9, Wakajihimu Jumapili saa11 alfajiri yeye ameshafufuka - Hayupo.

Mimi siropoki ropoki just noncence BLAH! BLAH!, Mathayo 12:40 inasema:

"Kwa maana kama vile Yona alivyokuwa ndani ya tumbo la nyangumi muda wa siku tatu, mchana na usiku, vivyo hivyo Mwana wa Adamu atakuwa ndani ya tumbo la dunia siku tatu, mchana na usiku."

Kwa akili ya kawaida kutoka Ijumaa Saa9 jioni hadi jumapili saa11 asubuhi hizo ni siku3 mchana na usiku kama alivyodai?

Hayo siyo masaa 38 au 39 hivi?

Je siku tatu mchana na usiku ni masaa 37, 38 au 39?

Je, Yesu siyo Muongo?

Kama ni muongo ataadhibiwa na nani?

Tuache hilo sababu sio point tunayoijadili.

Swali kwako: Kama unaamini Mungu ndiye muumbaji lakini unakataa dai kwamba hajauumba umasikini duniani bali kaumba utajiri pekee, Je umasikini umetokea wapi?

Nani kauumba umasikini?
Mkuu uko na mambo heavy kabisa 🤣

Hizi dini hizi bhana dah
 
Achana na hizo hekaya uchwara za Zaburi sijui kuinuliwa.

Haya maisha kila kitu ni bahati, then inafuata bidii na juhudi.

Kuna watu wamepata bahati ya kuzaliwa familia za kitajiri hivyo juhudi kidogo tu. Anatoboa.

Kuna watu wanazaliwa kwenye familia za kimaskini pangu pakavu tia mchuzi, Hadi uje utoboe utatia bidii na juhudi mpaka utoke jasho la meno.

Na bahati isipokuja upande wako unabaki kwe cylce ileile ya umaskini.
 
Back
Top Bottom