Zaburi 113:7: Humwinua fukara kutoka mavumbini, humnyanyua maskini kutoka unyonge wake

Sasa lini? Mbona miaka inakatika sioni maajabu?
Huyo hiyo mali hajatafuta yeye, kaikuta tu! Walioitafuta hiyo ndio walipata shida kwa kupitia changamoto kama unazopitia wewe! Pengine ni babu wa babu yake! Hivyo na wewe fanyakazi kwa bidii ili kizazi chako kije kufurahia matunda yako!
 
Huyo hiyo mali hajatafuta yeye, kaikuta tu! Walioitafuta hiyo ndio walipata shida kwa kupitia changamoto kama unazopitia wewe! Pengine ni babu wa babu yake! Hivyo na wewe fanyakazi kwa bidii ili kizazi chako kije kufurahia matunda yako!
πŸ‘ πŸ‘ πŸ‘
 
Nimejifunza mambo haya katika maisha yangu, Mche Mungu wako, epuka kutenda dhambi, wapende watu wote pamoja na familia yako, toa msaada pale unapoweza, jaribu kuondoa uchungu kwenye moyo wako, wasamehe watu waliokukosea, jaribu kufurahi na kuwa na amani na watu wote na mwisho mwombe sana Mungu akusaidie kushinda vishawishi vya shetani maana ni vingi sana.
 
E mkuu umepiga pakubwaπŸ˜€
 
Ufanye kazi sio utegemee zaburi. Hamchelewi kukalisha kombwe na kuzuia akili kuwaza kutatua changamoto za maisha mkisubiri zaburi itimie.
Ukafanye kazi sio usubiri muujiza wa kuinuliwa. HAta mtunga zaburi alifanya jitihada hakukalisha kombwe
 
Mkuu uko na mambo heavy kabisa 🀣

Hizi dini hizi bhana dah
 
Achana na hizo hekaya uchwara za Zaburi sijui kuinuliwa.

Haya maisha kila kitu ni bahati, then inafuata bidii na juhudi.

Kuna watu wamepata bahati ya kuzaliwa familia za kitajiri hivyo juhudi kidogo tu. Anatoboa.

Kuna watu wanazaliwa kwenye familia za kimaskini pangu pakavu tia mchuzi, Hadi uje utoboe utatia bidii na juhudi mpaka utoke jasho la meno.

Na bahati isipokuja upande wako unabaki kwe cylce ileile ya umaskini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…