Zacharia Isaay (Mbunge Mbulu): Serikali iache kigugumizi ieleze wazi kuhusu ugonjwa wa kupumua unaomaliza watu wa Mbulu

Zacharia Isaay (Mbunge Mbulu): Serikali iache kigugumizi ieleze wazi kuhusu ugonjwa wa kupumua unaomaliza watu wa Mbulu

kwani huyu mbunge ni mtaalamu wa afya? Tunao wataalamu kwenye wizara husika, tuna Dr. Gwajima, Dr. Mollel nk. Hao kama kiutaalamu hawajaona tatizo basi asiye mtaalamu atalionaje? Vinginevyo tukubaliane na wabunge waliosema wasomi (kwa vyeti) 'wanaliagusha' taifa, na labda basi na hao wa wizara hii wamo.
Na kama yule aliyeshindwa kuapa tulidoubt elimu yake, je hao wa afya tunawaamini vipi?
Sasa mtu kama Mollel ni mng'oa meno atajuaje watu wanao ugua corona? Labda jino lilio toboka..
 
Awe ametaja neno corona au hajataja, hoja yangu ni kuwa watu wamekuwa na woga wa kijinga mpaka kufikia hatua ya kuogopa kutaja mambo yaliyopo. Kwangu mimi huyo siyo jasiri bali ametimiza wajibu wake. Hata kama wengine wameogopa lakini hakumfanyi awe jasiri.
Huyo Mbunge ni jasiri, acha ubishi buda
 
Wewe ndiye mpumbavu kabisa.
Una haki kabisa kutetea unayemtetea. Alikunusuru na tetemeko lililojinyofolea roho kumi na saba za watu. Ni wajibu wako mtoto wa kijiji cha Katerero kwenye mto Ngono kuteta na anayeteta na mkombozi wako!
 
Tunaishi kwa neema hakuna anayepaswa kujidai eti ati anaomba Sana kuzuia Corona! Mungu peke yake ndiye anastahili sifa anayeshikilia uhai was mtu tajiri,maskini,mjanja,mwerevu,mwema,mdhambi,mstarabu,mpumbavu,awe wa rangi gani hakuna aliye na kinga ya kukwepa tumshukuru na kumwomba Sana Mungu ila siyo kujihesabia haki eti una uwezo wa kuzuia balaa! Uwezo huo Ni wa Mungu tu!
IMG_20210209_112054_0.jpg
 
Huyo Mbunge ni jasiri, acha ubishi buda
Of course kundi la watu waoga nalo lina jasiri wake! Watu waoga walikuwa ndani usiku wamelala, paka akapita na kugusa mlango, wote wakaingia uvunguni mwa kitanda kujificha, kasoro mmoja aliyebaki kitandani kupiga kelele kwa woga. Asubuhi yake ilipogundulika ni paka wakawa wanamsifu yule aliyepiga makelele ya woga kuwa ni jasiri.
 
Back
Top Bottom