Zahera: Hakuna mchezaji wa Yanga anaweza kucheza Pyramid FC. Tulisajili kwa ajili ya Ligi Kuu sio Klabu Bingwa Afrika

Zahera: Hakuna mchezaji wa Yanga anaweza kucheza Pyramid FC. Tulisajili kwa ajili ya Ligi Kuu sio Klabu Bingwa Afrika

aende tu Hana ajualo msanii tu
Na kama hataondoka sasa huyu timu itamfia mikononi mwake huyu hiyo ligi yenyewe anapigwa tu
 
Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa hawezi kuwasikiliza mashabiki wanachokisema kwa sasa baada ya kufungwa na Pyramids FC bali anawasiliana na uongozi ambao ulimpa mkataba.

Hayo yamekuja kufuatia mashabiki wa klabu hiyo kutoa malalamiko yao wakimtaka Zahera kuondoka kutokana na matatizo wanayosema yamekithiri kwenye kikosi ikiwemo kushindwa kupanga vizuri kikosi cha kwanza pamoja na mbinu.

"Mimi sikuajiriwa na mashabiki wa Yanga bali nilisaini mkataba na viongozi, kwahiyo siku viongozi wakinitaka kiwaachie timu nitafanya hivyo, sitokwenda mazoezini", amesema Zahera.

"Nina uzoefu mkubwa ila hapa Afrika, mashabiki wanakasirika. Hakuna mchezaji yoyote wa Yanga anayeweza kucheza Pyramids FC na lingine ni kwamba wakati tunasajili wachezaji, hatukusajili kwa ajili ya Klabu Bingwa Afrika ila tulisajili kwa ajili ya ligi", ameongeza.

Aidha Zahera amesema kuwa mashabiki hawapaswi kumlaumu yeye kwa matokeo ya Klabu Bingwa kwani kikosi chake kiliandaliwa kwa ajili ya ligi kuu, ambako hawapo katika nafasi mbaya mpaka sasa, wakiwa wamecheza mechi chache.

Yanga inatarajia kusafiri hadi nchini Misri kuvaana na Pyramids katika mchezo wa marudio utakaopigwa wikiendi hii, ikiwa nyuma kwa kufungwa mabao 2-1.
Yanga wajeuri huu ni ukweli mtupu kabisa ameongea mzee wangu Zahera
 
Tumezoe kuishi kwa mihemuko, ni ukweli mtupu kwamba siyo tu yanga timu yoyote ya Tanzania inge pangwa na pyramid isingefua dafu. Lakini kwa kuwa Wabongo tu nataka mafanikio kwa njia rahisi ndiyo maana kocha hatufai. Pia wanayanga wametegwa na jirani wakaingia, vyombo vya habari vimeongoza katika hiyo kampeni ovu hasa ukizingatia kocha kiswahili chake ni cha ku jumlisha. Wame kuwa waki muuliza maswali mengi ya ovyo.
Kocha mkweli sana huyu. Msimu uliopita tuliona Timu inashindwa hata kulipa mishahara ya wachezaji, hadi kina Dante hadi leo wapo mtaani. Usajili ulifanyika kabla ya CAF haijatupatia nafasi 4 za ushiriki wa timu zetu. Yanga mkimtimua kocha Zahera laana yake itawaandama.
 
Investment yenu ikoje?
Mimi ni mmoja WA watu waliokuwa wakimuamini Sana zahera,lakini sasa nimeamini huyu kocha ni porojo mingi hii ni timu kubwa na hakikuandaliwa kwa ajili ya ushindi WA ligi ya ndani tu tunaitaji ushindi,asituone tunambabaikia ........
 
Kocha muongo
YANGA WAMEPEWA TAAARIFA YA KUSHIRIKI CAF TAR 4_6_2019 usajili umefungwa 31july
 
Yanga kikosi cha ushangiliaji au ndio timu ya mpira, kama simba queens au?
 
Tangu siku ya Kwanza namuona huyu jamaa kwenye mahojiano niliona hakuna kitu hapo,
 
Kocha mkweli sana huyu. Msimu uliopita tuliona Timu inashindwa hata kulipa mishahara ya wachezaji, hadi kina Dante hadi leo wapo mtaani. Usajili ulifanyika kabla ya CAF haijatupatia nafasi 4 za ushiriki wa timu zetu. Yanga mkimtimua kocha Zahera laana yake itawaandama.

Huyu kocha ana mazur na mabaya yake...Mazuri yake ni kuwa ni mhamasishaji mzuri na yuko tayari kufanya kazi katika mazingira magumu na pia ni muumini wa nidhamu ya wachezaji...lakini mabaya yake ni kuwa he talks a lot au kwa maana halisi ni mropokaji...Nadhani Yanga haiwahitaji waropokaji...
 
Ndio mnashtuka eeh,mwaka Jana alikuwa akikarabia kucheza na Simba anawaandaa kisaikolojia vyura ,kuwaSimba ipo vizuri Kila eneo.Alipojitahd kutoa droo
Akaanza kuiponda Simba...ila sio Siri kwa namna alivoibeba Yanga Mwaka Jana...inatakiwa uwe na roho ngumu kumtukana!
 
Zahera out...ana chuki na baadhi ya wachezaji kama Balinya...alafu ana dharau sana .wakati Dasabre kocha wa Pyramids kawasifia sana Fei na Tshishimbi it means aliona kitu kwao lenyewe linabwabwaja hakuna mchezaji wa kucheza Pyramids
 
Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa hawezi kuwasikiliza mashabiki wanachokisema kwa sasa baada ya kufungwa na Pyramids FC bali anawasiliana na uongozi ambao ulimpa mkataba.

Hayo yamekuja kufuatia mashabiki wa klabu hiyo kutoa malalamiko yao wakimtaka Zahera kuondoka kutokana na matatizo wanayosema yamekithiri kwenye kikosi ikiwemo kushindwa kupanga vizuri kikosi cha kwanza pamoja na mbinu.

"Mimi sikuajiriwa na mashabiki wa Yanga bali nilisaini mkataba na viongozi, kwahiyo siku viongozi wakinitaka kiwaachie timu nitafanya hivyo, sitokwenda mazoezini", amesema Zahera.

"Nina uzoefu mkubwa ila hapa Afrika, mashabiki wanakasirika. Hakuna mchezaji yoyote wa Yanga anayeweza kucheza Pyramids FC na lingine ni kwamba wakati tunasajili wachezaji, hatukusajili kwa ajili ya Klabu Bingwa Afrika ila tulisajili kwa ajili ya ligi", ameongeza.

Aidha Zahera amesema kuwa mashabiki hawapaswi kumlaumu yeye kwa matokeo ya Klabu Bingwa kwani kikosi chake kiliandaliwa kwa ajili ya ligi kuu, ambako hawapo katika nafasi mbaya mpaka sasa, wakiwa wamecheza mechi chache.

Yanga inatarajia kusafiri hadi nchini Misri kuvaana na Pyramids katika mchezo wa marudio utakaopigwa wikiendi hii, ikiwa nyuma kwa kufungwa mabao 2-1.
kwani zahera bado ni kochatu jmn
 
Huyu kocha inabidi afukuzwe haraka sana. Kwanza Mara aseme wachezaji wa yanga viwango vyao ni vidogo sana kulinganisha na pyramids, Mara aseme yanga walifungwa kwa bahati mbaya. N way huyu kocha naamini hana ujuzi wa kufunza mpira ndio mana yanga wanacheza hovyo kuliko timu yoyote kwenye ligi ya bara
 
Back
Top Bottom