Zahera ni Mkongo aache kuzisemea timu za Tanzania hazimuhusu

craq

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
859
Reaction score
1,866
Mwisho wa kunukuu msemaji mwenye IQ ndogo wa simba amesema hivi mbele ya kituo cha Radio.


Wadau wa michezo naombeni mchambue na mdadavue hii kauli ya msemaji wa simba.

Uwanja wenu
 
Sijawahi kumkubali huyu msemaji wetu, yaani yeye anatafasri usemaji kavu kavu bila kujua usemaji unatakiwa uwe vipi.

Kuna usemaji na uropokaji yule ni mropokaji wa SSC.
 
Mwisho wa kunukuu msemaji mwenye IQ ndogo wa simba amesema hivi mbele ya kituo cha Radio.


Wadau wa michezo naombeni mchambue na mdadavue hii kauli ya msemaji wa simba.

Uwanja wenu
Namkubali sana tena , anafanya kazi nzuri sana natamani awe msaidizi wa Polepole CCM, wapinzani mtapotea kabisa
 
Kati ya wasemaji wa ovyo kuwahi kutokea ni Haji Manara! Staili anayoitumia ya 'kubwabwaja' haina tija yoyote! Sababu tu amezaliwa katika familia ya soka ndio anajiona mjuaji kuliko wenzie
 
Mwisho wa kunukuu msemaji mwenye IQ ndogo wa simba amesema hivi mbele ya kituo cha Radio.


Wadau wa michezo naombeni mchambue na mdadavue hii kauli ya msemaji wa simba.

Uwanja wenu
Manara Uwezo wake wa kufikiri ni mdogo na hana heshma. Wakati yeye uwa ana lalamika watani zake wanapomwita zeruzeru jina ambalo anaona kama ni la kibaguzi katika jamii , yeye juzi anazungumza kwenye kituo cha redio akisema Zahera ni Mkongo hastaili kuzungumzia mambo fulani katika soka la Tanzania.
Ana sahau kwamba watu wa Soka ni familia moja na ndio maana Goli linafungwa katika ligi ya Venezuela linaingia katika kushindanishwa na magoli mengine bora dunian.
Manara kwa kauli aliyoitoa kwa Zahera ni ya ubaguzi katika soka. Zahera anaongea ukweli na kunasiku ataondoka na sisi tutaendelea na ubabaishaji wetu.
Vyombo vya habari za michezo vinatakiwa vimwambie ukweli Haji Manara, Kama yeye anavyo chukia kubaguliwa kwa kuitwa Zeruzeru na Yeye anafanya dhambi ya Ubaguzj kwa kumwita Zahera Mkongo na hastaili kuzungumzia mambo ya mpira wa nchi hii.
Ni jambo la aibu kwa Klabu kubwa kama ya Simba kuwa na msemaji mwenye mihemko na kauli za hovyo kama Haji manara.
 
Ni kweli, alichofanya Manara, ni zaidi ya ubaguzi au tuseme ni unyanuapaa. Zahera kasema kama mdau ktk mashindano Haya na kaweka hoja zake bayana pasipo uficho, Haji anamjibu kwa kumnyanyapaa, kwa hili anapaswa kuomba radhi wapenda soka na club take pia impe onyo kali juu ya ulopokaji wake usiyo na chembe ya ustaarabu. We don't want Racism in our country.
 
Mwisho wa kunukuu msemaji mwenye IQ ndogo wa simba amesema hivi mbele ya kituo cha Radio.


Wadau wa michezo naombeni mchambue na mdadavue hii kauli ya msemaji wa simba.

Uwanja wenu
Lete ushahidi kwanza Ndo tudadavue
 
Nahisi Manara na wanaomuunga mkono wana tatizo la kujua tofauti baina ya Msemaji wa Klabu, Mhamasishaji na Afisa Habari. Pengine hata wanaomlaumu nao wanafanya kosa hilohilo. Kwanza tunapaswa kutofautisha, kwa sababu Manara mwenyewe ameshindwa kutofautisha, baina ya Haji Manara na Msemaji/Afisa Habari wa Simba. Haji Manara hafungiki kutoa maoni yake binafsi kwenye swala lolote lile, lakini anapaswa kutoa angalizo mapema kabla ya kutoa kauli kama hiyo. Lakini anapaswa pia kuchunga kauli zake kama Manara, kwa kujua kwamba hata akitoa angalizo mapema, kauli yake yoyote tata lazima itaishia kuhusishwa na Simba kwa sababu yeye ni kiongozi wa Simba. Na Bado inatuwia vigumu kumhukumu dhidi ya matendo na maneno yake viwanjani na kwenye vyombo vya habari kwa sababu hatuelewi maelezo ya kazi (job description) yake. Msemaji wa klabu, mathalan anategemewa kutumia zaidi kalamu a mdogo waku kuliko kiuno chake, kwa hivyo hategemewi kuonekana ‘anamwaga radhi’ uwanjani mbele ya washabiki wa timu yake. Lakini mhamasishaji anakubalika kufanya hayo. Kadhalika Afisa habari, anategemewa zaidi kuwa msimamizi wa vyombo vya habari vya klabu (radio, TV, mitandao ya kijamii, n.k. na si kuwa ndiye mwenye mitandao hiyo ya kijamii au kuwa ndiye mtangazaji kwenye vyombo hivyo vya habari.
 
Mi naona shida kubwa ya Manara ni kutojiamini na anatafuta sana kuaminiwa huwa nafuraha sana anaposifiwa na ni muoga sana wa kukosolewa
 
Mi nadhani Aden Rage alipowaita Mbumbumbu itakuwa alimaanisha Haji Manara maana alisema baadhi yenu.
 
Kwani mlitakaje ?aseme Zahera ni mTz...!uhalisia ni kuwa Zahera ni mkongo,na hivyo ndivyo alivyosema..!msubiri kipigo cha mbwa koko this time!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…