Yule alianzisha Vita dhidi ya Wapinzani na Wafanyabiashara wa Tanzania akidai kuwa ndio Maadui kumbe lengo lilikuwa ni kuwakaribisha ndugu zake waje kutake over.Nasikia wabongo wengi malori wameyakimbiza Zambia ,Zimbabwe ,Malawi na Congo , wengine wameenda Hadi South Africa , biashara zimedoda hapa na pia kipibdi like cha vurugu za kukamatana na kutekana Kwa visingizio vya uhujumu uchumi
Kuna tajiri mmoja yupo mwanza, akiwa na mzigo wa kuja kubeba Dar, hayatembei yote, mengine hubebwa na wenzao, ili kubana matumizi ya mafuta.haya maroli yaliyobebana mawili mawili hayana containers ni flat beds
Tazara inawatosha itumieni vzr.Maroli yanayorudi tupu na hadi mengine kubebana ni yale yanayotokea mwanza burundi uganda na rwanda , na ndo huko sgr imepelekwa.
Unatakiwa ujiulize pia hiyo Sgr itarudi na mzigo upi!
Maroli ya kusini juu mbeya sumbawanga nk hayajawai kurudi tupu dar
Maroli kutoka mombasa hadi naivasha hayafanyi kazi tena kwa sababu Sgr yao ime hit the right target,Tazara inawatosha itumieni vzr.
#MaendeleoHayanaChama
Serikali haina ubunifu katika uzalishaji. Ni wataalamu wa kukopa simply kuna 10% wanawekewa kwenye account zao nje, posho kubwa waendapo nje kusign hiyo mikopo. Kifo cha viwanda vya ndani na nguvu ndogo kuweka mikakati ya kilimo ni ushahidi tosha. Wastaafu wana pesa na ujuzi wa kuanzisha miradi, lakini ndio wanafia maofini kwa teuzi. Walio maliza vyuo jana hawana mitaji na uzoefu ndio wanaambiwa wajiajiri. Matokeo wanaishia kuwa wamachinga, wachuuzi wa bidhaa za China.Ni mekuwa najiuliza hii misururu mirefu ya maroli yanayorudi Dar ikiwa tupu na mingine kubebana miwili, hivi hatuna bidhaa za kupeleka bandarini? hatuna marobota ya pamba katani kahawa mahindi alizeti mashudu? ni kweli hatuna bidhaa za kuuza nje ya nchi? sie tumekuwa soko la bidhaa za nje tu?
Naimani haya maroli yalienda mikoani yakiwa na bidhaa kufika huko yalikosa mzigo wa kuridi nao hivyo kuamua kurudi tupu na mengine kubebana kama panzi.
Nilitegemea maroli yatoke tupu Dar yafuate mzigo mikoani, yafuate ngozi pamba katani mashudu ng'ombe. Kama uchumi wetu ni kuagiza tu sie tunauza nini? trade balance yetu ikoje? Raisi anatoa wapi fedha za kigeni kukidhi mahemezi yetu?
Kwanini yasiruhusiwe japo kubeba mbuzi na michele kukawa na ushindani nyama ikashuka bei kwa kushindanisha transportation costs?Inawezekana yakarudi tupu kwa sababu malori yaliyoandikwa TRANSIT ubavuni kwa namna yoyote hayaruhusiwi kubeba mzigo wa ndai ya nchi. Yakipeleka mzigo nje ya nchi yanatakiwa kupakia pia huko huko ile yaje na mzigo.
Ukiona yako tupo angalia ubavuni. Kama yameandikwa TRANST basi yanakuwa yamekosa mzigo kule yalikoenda au ameamua kuwahi mzigo mwingine DAR.