Zaidi ya 90% Ya Marais Wote Duniani Wamegoma Kumpongeza Samia Kwa Ushindi Ukilinganisha Na Mtangulizi Wake

Zaidi ya 90% Ya Marais Wote Duniani Wamegoma Kumpongeza Samia Kwa Ushindi Ukilinganisha Na Mtangulizi Wake

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Wengi tulizoea kuona Viongozi wa kidunia wakiwapongeza Marais wa Tanzania pale wanaposhinda chaguzi, na wengi mnakumbuka mwaka 2015 na 2020 tulishuhudia Viongozi wa kidunia wakiwemo Marais, Wawakilishi wa Marais, Wakuu wa Taasisi na mashirika ya kidunia wakitoa Pongezi zao kwa Rais wa Tanzania pale anaposhinda uchaguzi.

Lakini kwa Samia imekuwa jambo la kushangaza ambapo mpaka sasa ni zaidi ya 90% ya Viongozi hao wa kidunia hawajampongeza wala kuhudhuria kuapishwa kwake. Kwa Ulaya ni nchi ya Urusi pekee iliyotuma pongezi, lakini Viongozi wengine wote wapo kimya. Hata nchi kama Nigeria zilizozoea kutuma wawakilishi na wao hawajatuma hata diwani wa Lagos.

Umoja wa Afrika umetangaza kwamba uchaguzi uliofanyika Tanzania haukuwa wa kidemokrasia, na 90% ya marais wa Afrika walikataa kumpongeza Samia Suluhu Hassan kwa “ushindi” wake wa urais wakati Tanzania imekuwa jadi kupokea pongezi kama alizopata Magufuli 2020. Hii pia inahusisha viongozi wa Asia, Ulaya, Amerika, na Australia, wakiwemo wakoloni wetu Ujerumani na Uingereza wote wamekausha.
 
Watu duniani walishaacha kuuawa kisa madaraka watapongezaje mauaji mzee
 
Pongezi sio lazima hadi Lissu asikie na aje kusema Rais Samia kapongezwa, na kapongezwa sana
 
Pongezi sio lazima hadi Lissu asikie na aje kusema Rais Samia kapongezwa, na kapongezwa sana
Wewe Ubongo wako umepata Cancer inayoitwa Lissu... unahitaji tiba, maana jamaa kafungwa lakini bado ubongo wako unakereketwa na jina lake

Au wewe ni Fisiemu
 
Namana hata kiduku wa pale N.K amegoma kutuma salamu, ataingia kaburini na msongo mkubwa wa mawazo hataisahau hii, damu za watu wasio na hatia zinamlilia kila uchwao.
 
Back
Top Bottom