Zaidi ya bilioni 200 kutumika kutandaza mkongo wa Taifa wa mawasiliano wenye urefu wa 4244km kwa kutumia miundombinu ya TANESCO

Zaidi ya bilioni 200 kutumika kutandaza mkongo wa Taifa wa mawasiliano wenye urefu wa 4244km kwa kutumia miundombinu ya TANESCO

Habari za kujengwa kwa mkongo wa taifa na kuanza kutumika zilikuwepo toka Kikwete akiwa anaingia madarakani. Pesa zikatolewa na ujenzi wa huo mkongo ukaanza kipindi kile kile. Mpaka leo hii ni hadithi tu za kusadikika kuhusu faida tulizohaidiwa. Ni sawa sawa na ule ujenzi wa bomba la gesi la Mtwara na faida zake. Ni upigaji mtupu.

Sasa leo tena tunasikia ujenzi wa mkongo wa taifa! Sijui tunarudia kujenga?
Muda usio mrefu tutasikia tena tunaanza ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara.
 
Watueleze faida za mkonga tofauti na zile zilizozoeleka. Mara nyingi hiyo miradi huja kuongezwa gharama za maisha kwa mwananchi wa chini.

Ikiwezekana waachane na hizo fedha na zielekezwe kwenye sekta nyingine kama vile barabara
 
Umeme bado tatito ,je hiyo fiber to home itakuwaje.
 
ZAIDI YA BILIONI 200 KUTUMIKA KUTANDAZA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO WENYE UREFU WA 4244KM KWA KUTUMIA MIUNDOMBINU YA TANESCO

"Tunamshukuru sana Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha zaidi ya bilioni 200 kwa lengo la kutandaza Mkongo wa taifa wenye urefu wa 4244Km kwa kushirikiana na Shirika la umeme Tanzania (TANESCO). Mradi huu utapunguza kwa kiasi kikubwa gharama za huduma za Mawasiliano Tanzania na kufikisha huduma za intaneti kwa maeneo mengi Nchini kwa kutumia mradi unaojulikana kwa jina la "FIBER TO HOME kwa sababu Mawasiliano ni haki ya kila Mtanzania na lazima yafike Nchi nzima ". - Ameyasema hayo Mhe. Dr. Faustine Ndugulile Waziri wa Mawasiliano na technolojia ya habari wakati wa halfa ya utiaji saini Mkataba Kati ya Wizara ya Mawasiliano na teKnolojia ya habari na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Ujenzi wa Miundombinu ya Mkongo wa taifa wa Mawasiliano kwa kutumia miundombinu ya umeme. Leo jijini Dar es Salaam

View attachment 1928034
View attachment 1928036
View attachment 1928037
View attachment 1928038
View attachment 1928039
View attachment 1928040
Hizi pesa ni nyingi kama kweli zitaleta tija na nafuu inayokusudiwa.Maana Mwigulu na Ndungulile wamekuwa wakipigia chapuo hili kwamba litashusha gharama za data nk.

Ila sasa na wewe Waziri uache mentality za kimwendazake ,sema tuu unaishukuru Serikali ya awamu ya 6 kwa kutoa pesa kwa ajili hiyo.Mambo ya kumshukuru Rais kama personal sio sawa.

Mwisho shida ya nchi yetu sio pesa bali vipaombele vyenye kuleta tija.
 
Good idea! TTCL hawana miundo mbinu ya kutosha ndo maana hata utandazaji wake ukaishia kwenye baadhi ya sehemu tu! Sasa sijui kuna technlojia ipi, lakini kama inawezekana kutandaza mkongo wa mawasiliano kupitia lines za TANESCO, na kwavile TANESCO imeenda hadi vijijini, basi usambazaji wake utafika mbali zaidi kuliko ilivyokuwa upande wa TTCL

Hata hivyo, interest yangu sio kushuka bei, kwa sababu I bet haitashuka lakini angalau huduma itaweza kupatikana hadi vijijini
Kama ni wa TTCL bei zitashuka maana maofisini ile wifi yao iko chini Sana,imagine nchi nzima kufikiwa .

Turudi nyumbani kumenoga.
 
Watueleze faida za mkonga tofauti na zile zilizozoeleka. Mara nyingi hiyo miradi huja kuongezwa gharama za maisha kwa mwananchi wa chini.

Ikiwezekana waachane na hizo fedha na zielekezwe kwenye sekta nyingine kama vile barabara
How? Ungekuwa unafanya Kazi ofisi za umma ungeelewa.
 
Wajinga wanachekelea tu washajisahau😅 tena yani Watanzania vichwa panzi sana!

Hizo Billion 200 lazma mzichange tena. Utaskia siku sio nyingi kila mwenye line atakatwa buku kila mwezi ili kuchangia usambazaji wa Mkongo wa taifa!😂 Tujiandae kisaikolojia yani kama si 1GB kuuziwa elfu 4 bila soni
Pesa zipo zimetolewa acha kupayuka.Tena hizi pesa ni sehemu ya ule mkopo walisaini majuzi,shida yenu mumekaa kupinga kila kitu hakuna mnachoona.

Tzn ni moja ya nchi ziko mwishoni kwenye penetration ya mambo ya ICT na ku digitalize uchumi,sasa kwa hili means linaenda kuongeza huo wigo na kuleta nafuu ya data.

Mathalani kampuni za simu zikitumia mkonga huu kwa bei nafuu bila shaka hata huduma zao kwa wananchi zitakuwa nafuu pia.
 
Aliyekwambia bei itakuwa nafuu ni nani?😎 Ache kujitekenya na kucheka mwenyewe
 
Aliyekwambia bei itakuwa nafuu ni nani?😎 Ache kujitekenya na kucheka mwenyewe
Nakuuliza na wewe,umewahi fanya Kazi ofisi yoyote ya serikali?

Kule kuna wife za TTCL zilizounganishwa na hiyo cables, gharama za data ni chini Sana,kasi kubwa kuliko mitandao mingine hii inayotegemea satellite.

Kwa mfano 4G iko expensive kuliko kutumia cables nk.
 
Hivi unajua cost ya kujiunga na home wifi kwa TTCL around laki 8 kwa mwezi? Ila mitandao mingine ni less than that? Around 200-400k!

How do you justify cheapness kwa hali hiyo?
 
Hivi unajua cost ya kujiunga na home wifi kwa TTCL around laki 8 kwa mwezi? Ila mitandao mingine ni less than that?
Ni kwa sababu base yao ilikuwa ndogo lakini saizi Wana boost uwezo bila shaka na gharama zitapunguzae kiasi ,tusubirie mradi uishe majibu yatapatikana.
 
ZAIDI YA BILIONI 200 KUTUMIKA KUTANDAZA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO WENYE UREFU WA 4244KM KWA KUTUMIA MIUNDOMBINU YA TANESCO

"Tunamshukuru sana Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha zaidi ya bilioni 200 kwa lengo la kutandaza Mkongo wa taifa wenye urefu wa 4244Km kwa kushirikiana na Shirika la umeme Tanzania (TANESCO). Mradi huu utapunguza kwa kiasi kikubwa gharama za huduma za Mawasiliano Tanzania na kufikisha huduma za intaneti kwa maeneo mengi Nchini kwa kutumia mradi unaojulikana kwa jina la "FIBER TO HOME kwa sababu Mawasiliano ni haki ya kila Mtanzania na lazima yafike Nchi nzima ". - Ameyasema hayo Mhe. Dr. Faustine Ndugulile Waziri wa Mawasiliano na technolojia ya habari wakati wa halfa ya utiaji saini Mkataba Kati ya Wizara ya Mawasiliano na teKnolojia ya habari na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Ujenzi wa Miundombinu ya Mkongo wa taifa wa Mawasiliano kwa kutumia miundombinu ya umeme. Leo jijini Dar es Salaam

View attachment 1928034
View attachment 1928036
View attachment 1928037
View attachment 1928038
View attachment 1928039
View attachment 1928040
Hili neno 'Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano' sio mara ya kwanza kusikika.
Lililiishasemwa miaka kama Sita au kumi hapo nyuma na wakaanza kuchimba mitaro kwa ajili ya kupitishia waya za Mkongo wa Mawasiliano.
Na ahadi ikawa ile ile kama zinavyokuwa Ahadi nyingine Zote feki...'Mkongo utarahisisha Mawasiliano na Kupunguza Gharama'!...[emoji848][emoji848]

Watuambie kwanza 'Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano' ule Uliishia wapi na huu ni Upi???[emoji848][emoji848]
 
Ngoja tutaona itakavyokuwa mradi ukikamilika. Rahafiber au Hai wanapima unlimited internet kuanzia 10Mbps kwa 60k. Labda huu wa serikali unaweza kuwa nafuu zaidi...
 
Bora tumsubiriage yule tapel wa Marekani wa Starlink Kama atafika huku Africa mashariki basi tutapata raha Ila sio wahuni wetu Hawa
Hahahahaha yani inashangaza sana wenzetu wananunua internet kwa bill kama maji sie kwetu tunauziana bundle kwa mafungu kama nyanya😅
 
Hahahahaha yani inashangaza sana wenzetu wananunua internet kwa bill kama maji sie kwetu tunauziana bundle kwa mafungu kama nyanya😅
So Bora hata nyanya, utadhani msimu ule wa maembe Kuna vijiji ukifika unakuta ndoo liter 20 ya maembe wanauza buku😂😂😂

Juzi Kati hapa nilijipendekeza kuulizia vsat ttcl hizo gharama zake nilirudi nyumbani kichwa kinauma mno 😢😢😢 utadhani nataka kuuziwa mnara wote daah
 
Hahahahahaha nilimwambia kenge mmoja anaesifia TTCL ukiomba unlimted yao ni wanauza karibia 1M!
 
Back
Top Bottom