MWANAHARAKATI MWEMA
JF-Expert Member
- Dec 16, 2022
- 216
- 313
Un
Rudia kusoma.utaelewa
nilichokigundua hapa Kuna mtu anataka amfunike mwendazake Ila mbinu anazotumia nyingi Ni kuongeza Deni na kupigwa Ni mwingi, usimamizi Ni finyu sana watu wanajifanyia TU.Napongeza hii initiative ya Serikali
Japo yatupasa kuwa makini na gharama Za wakandarasi kutokuwa kubwa kuliko bei ya soko.
Pili lazima reinforcements ya quality monitoring iwe na uwezo pia mamlaka ya kuhakikisha barabara zetu zinakuwa na ubora stahili (Value for Money).
Tatu,Nchi yetu tayari Ina undertake turnkey mega infrastructure projects (SGR,Stigler,BRT,Etc)..Kimsingi uchumi wetu umeelemewa sana..Hatukupaswa kuharakisha kusign mikataba ya kandarasi zote Kwa wakati mmoja..EPC+F ni mkopo (Mkandarasi anajenga mradi Kwa kukopa Kwa niaba ya serikali in which sense tukilipa tunalipa na riba zote involved na zaidi sana tukichelewa kulipa kuna penalties..
Nchi yetu bado ni Changa,Hatupaswi kuwa na haraka sana ktk ujenzi wa miradi ambayo ROI si ya muda mfupi..Modalities Za EPC+F makampuni yanakopa kwenye commercial banks (Local or International)..Kuna riba..
Nadhani tuendako kwenye infrastructure projects tuangalie uwezekano wa ku implement EPC+F yenye BOT Modalities (Build,Operate and Transfer) hivyo contractor anakuwa na perspective ya kibiashara pia hivyo Hawezi ku overcharge au kujenga mradi chini ya kiwango.
Nne,Miradi yote tajwa inajengwa kwenye ukanda wa madini ya thamani kubwa (Vito na Rare Earth Metals)..Wachina wanajua nini Tuko nacho chini ya ardhi kupitia espionage satellite zao hivyo haya makampuni mengi makubwa ni State Owned or affiliated (SOE) hivyo yana mission zaidi ya ujenzi wa barabara (Ktk Hili nashauri vyombo vyetu vya usalama kufuatilia hili na kuwezeshwa ili kuziba mianya mikubwa ya utoroshaji na uvunaji wa rasilimali Za nchi..
Mwisho,Utekelezaji wa mipango ya maendeleo iende sambamba na ujenzi wa mifumo ya uzalishaji mkubwa (Kilimo,Ufugaji,Viwanda) ili kunenepesha uchumi na kuwezesha serikali kulipa madeni makubwa yatokanayo na mikopo toka Bank Ya Dunia,Benki ya maendeleo ya Afrika n.k.