Zaidi ya majiko 452,445 yasambazwa bure kuchochea Nishati safi

Zaidi ya majiko 452,445 yasambazwa bure kuchochea Nishati safi

Mwakongo

Member
Joined
Jul 8, 2025
Posts
60
Reaction score
15
RAIS SAMIA NA MAPINDUZI YA NISHATI SAFI. ZAIDI YA MAJIKO 452,445 YASAMBAZWA BURE. LENGO KUPUNGUZA VIFO VYA WA KINA MAMA

Rais Samia kwa kutambua kwamba vifo vitokanavyo nishati hafifu ya mkaa na kuni kwa mwaka ni zaidi ya 33,000, au zaidi ya vifo vitokanavyo na UKIMWI nchini, Rais Samia agawa bure mitungi zaidi 452,445 ya gas kwa zaidi ya kaya 205,000 nchini kufikia 2024 ili kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi nchini.

WATANZANIA OKTOBA TUNATIKI ✅
GAS-BURE.png
NISHATI-SAFI.png
 
safi sana ila serikali ihakikishe na bei ya kujazia hizo cylinder inakuwa rafiki ili na wavijijini waweze kumudu hizo gharama na uchaguzi unakuwa huru na haki ukihusisha vyama vikuu vyenye nguvu ili atakayeshinda awe ameshinda kwa haki
 
Kumaanisha Mama yako alikufa kwa matumizi ya mkaa ? pole sn na Hongera kwa Bi tozo kuuokoa ukoo wenu usiendelee kuteketeketea..
 
safi sana ila serikali ihakikishe na bei ya kujazia hizo cylinder inakuwa rafiki ili na wavijijini waweze kumudu hizo gharama na uchaguzi unakuwa huru na haki ukihusisha vyama vikuu vyenye nguvu ili atakayeshinda awe ameshinda kwa h

Kumaanisha Mama yako alikufa kwa matumizi ya mkaa ? pole sn na Hongera kwa Bi tozo kuuokoa ukoo wenu usiendelee kuteketeketea..
Na wale Mama zako wakubwa.... wewe hujui hata unachochangia hapa pole
 
RAIS Samia hata kama atagombea 2030 Mimi nitamchagua tena
Hii nchi inasikitisha sana. Kwa nini tunafurahia ukweli unapofichwa mchana KWEUPE.? Hawa wamama wanaogaiwa mitungi ya gesi leo ikiisha wataweza kujaza tena? Kwa sh 23,000.?? Kumbuka kiwa hiyo gesi inatoka Ukreni China au Urusi. Sisi tuna natural gas mabilioni ya cubic fiti za ujazo ambazo ni swala la uwekezaji mdogo tuu watanzania wanaweza kunufaika kwa kutumia gesi kwa bei ya chini ya sh 10,000 kwa mwezi. Kama nia ni njema kwa nini hilo lisifanyike kwa , maslahi , mapana ya nchi. Sipati picha na siwezi kuelewa. Labda kama akili yako iwe na tatizo
 
Etih uwekezaji mdogo wewe aliyokuambia kuwa ni uwekezaji mdogo huo!!! Kila kitu ni michakato na Tunaimani na Wizara ya Nishati wanaendela kuweka Miradi sawa na kuhakikisha hata walio vijijini sana wataweza kulipia Gas. Ila kwasababu wewe unamchango mdogo kwa hii nchi na huoni Maendeleo yaliyopigwa na serikali chini ya Rais wetu Samia basi kaa ukiwa mzigo kwa familiar yako na kukalilishwa mambo ya kijinga na watu wenye manufaa ya kushibisha matumbo yao kwa kisingizio cha kujiita upinzani kumbe wanatumika vibaya ili kuchafua Amani ya nchi yetu.
 
Wazo ni zuri, nia ni njema isipokuwa sio suala endelevu kwa sababu ya OPEX...

Watu wengi hawana hiyo mitungi si kwasababu hawana uwezo wa kujitutumua kuinunua bali ugumu ni gharama za ku-refill...

Sote tunajua maisha ya kijijini watu hupika vyakula vigumu vigumu ambavyo huitaji nishati joto zaidi, mathalani kuchemsha maharage, kande, kusonga ugali n.k...

Suluhisho ni kuwa na kampeni endelevu ya upatikanaji nafuu wa LPG kama ilivyo kwa LUKU(sijui kama linawezekana), wakati huo huo kukazana ujenzi na usambazi wa mtandao wa CNG ingawa itachukua miaka si chini ya 15 kuenea nchi nzima (wameanza huko Lindi sijui na Mtwara na Dar kidogo sana)
 
Back
Top Bottom