JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mradi huo wa bandari mbili ulianza Mwaka 2019 na ulitarajiwa kumalizika Mwaka 2021 lakini baadaye yakafanyika mabadiliko na muda kuongezwa.
Sisi Wananchi wa hapa tukaanza kujua neema imekuja japokuwa tulikuwa na wasiwasi kuhusu bandari hizo kutokana na historia ya eneo hilo kuwahi kuwa sehemu ya Ziwa Tanganyika.
Ukipita eneo la Bandari zote hizo mbili kwa asilimia kubwa zipo ndani ya maji, kwa ufupi ni kuwa haiwezekani tena miradi kufanyika.
Inawezekana wanaweza kusema kina cha maji kimeongezeka lakini hilo walitakiwa kulijua mapema, wao ni wataalam kuliko mimi raia wa kawaida.
Hali ilivyo kwa sasa ni mbaya na wengi wetu tumelazimika kukimbia maeneo yote ya karibu na Bandari, maji amekuwa mengi.
Ninachokiwaza zile bilioni 30+ zilizotengwa kwa ajili ya maboresho inamaana ndio zimepotea hivyo?
Mimi sio Mkandarasi ila akili ya kawaida ilitakiwa kutumika, hapo ninavyoona kuna mambo mawili, inawezekana utafiti haukufanyika kwa usahihi, ndio maana mambo yameharibika au ulifanyika lakini Wakandarasi wakapuuzia utafiti na historia ya sehemu hiyo kujaa maji.
Ilivyokuwa wakati wa ziara ya Kinana, Tarehe 1, Steptemba 2022
~ Bandari ya Ujiji imedumaa tofauti na matarajio yetu wana Kigoma Ujiji
~ Kinana akagua mradi ujenzi wa Gati la Bandari ya Ujiji Mkoani Kigoma, Septemba 1, 2022
~ Rais Samia aweka Jiwe la Msingi Mradi wa ujenzi Makao Makuu ya Bandari ya Ziwa Tanganyika, Oktoba 18, 2022