Zalisha faida kwa uwekezaji mdogo katika UTT na Hati fungani

greater than

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
1,653
Reaction score
3,060
Nipo zangu katika Site ya ujenzi ,Kuna wazo la Uwekezaji mdogo limenijia.
  • Kwa wale wanaopokea mshahara wa kuanzia 250,000 hadi 450,000
  • Ambao hawapati nafasi ya kufanya biashara nje ya kazi yao.
  • Wasio na Pensheni.
  • Uwezo wa kuiweka hela na kuisahau.
  • Fedha yenye maremgo ya miaka miaka mitano ijayo.

Fungua akaunti kwenye UTT
  • wekeza kwenye mfuko wa UTT,ambapo kima cha chini ni 100,000 ili uweze kuwekeza
  • Kila mwezi peleka 50,000 kwa mda wa miezi 20 (mwaka na miezi nane)
  • Jumla utakuwa umwekeza 1,100,000
  • UTT utazalisha faida ndogo ya 120,000 kutoka UTT
  • jumla utakuwa na 1,220,000
  • toa 1,120,0000 halafu kwenye UTT ubakishe 100,000
Nenda na uwekeze hiyo 1,120,000 kwenye hati fungani
  • Chagua hati fungani ya miaka 15 yenye kutoa Riba ya 13.5%
  • Kila mwaka utapewa 166,000 kwa mda mda wa miaka 15
Hiyo 166,000 ya kila mwaka kaiwekeze kwenye akaunti ya mtoto Benki au UTT...
  • Kwa mzunguko mmoja utakuwa na 166,000
  • Katika mzunguko wa pili ,Ukawekekeza 50,000 kila mwezi kule UTT kwa mda wa miezi 20 tena,na kuchukua hati fungani mpya utakuja pata 166,000 nyingine.
  • kwa mda wa miaka miaka 7 na nusu unaweza kuwa na mizunguko mitatu ambayo kila mmoja inazalisha 166,000 kwa mwaka kwa mda wa miaka 15.
Yaani, 166,000 x 3 x 15 = 7,470,000 ambayo ni faida ya Hati fungani.

Lakini kumbuka uliwekeza
100,0000 = ya kufungulia akaunti ya UTT
1000,000 x 3 = ya mzunguko (ule mchango wako wa 50 kwa mwezi kwenda UTT) X 3 (idadi ya mizunguko)
Jumla ya uwekezaji =3,100,000

Kwa ujumla utakuwa na 10,570,000

maoni na nongwa.....
 
Niombe kuuliza, nikiwa na M20 ni wapi naweza pata faida ya haraka kati ya UTT na hati fungani. Pia niombe kujua risks zinazoambatana na kila option.
 
Niombe kuuliza, nikiwa na M20 ni wapi naweza pata faida ya haraka kati ya UTT na hati fungani. Pia niombe kujua risks zinazoambatana na kila option.
Hati fungani ........tena chukua ya miaka 15,,,,Utapata Riba ya 13.54%...

The only ni pale serikali ikija firisika....
Though deni lako litasogezwa mbele...
 

Kaka ulichokieleza ndio kuna mtu kakifanya, sema yeye kaisusa 100M kwenye GovtBond, ambapo anapata 15+m kwa Mwaka kwa 13.5% , kisha akaweka
Standing order bank hiyo 15M ikiingia tu inapelekwa UTT .. sasa piga ndan ya 12 yrs hiyo 100m itakuwa umemzalishia ngapi.. ni almost nusu bilioni

Amesema amefanya hivyo kujiandalia mafao ya kustaafu nje ya nssf yake
 
Naomba kujua Kwa Kwa nini uweke kwenye Hati fungani ya miaka 15 (hapa hata pesa Yako ukiitaka ikiwa umepata dharura huwezi ipata for free), Si Bora uweke mfuko wa liquid ambao unatoa riba karibia sawa ukiwa na advantage ya kuchukua pesa Yako ndani ya siku 3 for free?

Assume umepata ugonjwa ambao
unahitaji gharama kubwa za matibabu, utaacha ufe kisa umewekeza Hati fungani?
 
Huu uzi nimeuelewa sana mkuu, hizi do miongoni mwa sababu chache zinazofanya matajiri waendelee kuwa matajiri zaidi.
Then naomba kujua, inawezekana kuwithdraw pesa yako uliyoiwekeza kwenye bond kabla ya muda wake wa maturity?
 

Kaka ni swala la malengo.. yeye amejiwekea kuwa hiyo 100m ni kukuza mtaj kwa ajili ya maisha ya kustaafu maana ana kama 10 years za kufanya kazi alivyojipangia Mungu akimweka hai na afya njema

Amesema hata ikitokea dharura atakopa.. ila anataka awe na 500m plus kwenye 2032/33

Ila pia uko sahihi angeweza kuweka jikimu na kupata gawio la kila miez 3 au bond akapata kila mwezi

Ila kumbuka jikimu ukiweka 100m.. kila Baada ya miez 3 utaondoka na 1.5m au 1.7m yaan ni sawa na 550k au 570k kwa mwez.. usifikiri jikimu itakupa 1m kwa kila Mwez kwenye 100m yako.. hata Bond haikupi 1m kwenye 100m yako utapata 850k hv kiufupi kwa Bond na jikimu itakuwa inakupa magawio kati ya 7% hadi 8.6% zingine zinarudishwa akukuza mtaji
 
Mpendwa Mwekezaji

Je! Muda wote umekuwa ukitafuta njia ya kujiongezea kipato cha uhakika kila mwezi, lakini kila unachojaribu kinashindikana?

Lakini vipi kama kuna njia rahisi, isiyo na usumbufu, inayokuwezesha kupata kipato cha uhakika kila mwezi kwa miaka 15 ijayo bila hata kumiliki nyumba ya kupangisha?

Embu Jaribu Kufikiria hili...

Unaamka kila siku ukiwa na uhakika kwamba kila baada ya miezi sita, akaunti yako ya benki inajazwa pesa bila kulazimika kufanya chochote.

Wewe unakuwa Unapata tu Kodi kama mwenye nyumba anavyokusanya kodi kila mwezi, Lakini bila hata kuwa na nyumba!

Yes Hii inawezekana Wala Hii siyo ndoto !

Kwani Ndani ya sekunde 60 zijazo utaenda Kugundua Jinsi ya Kupokea Kodi Yako mwenyewe kama mmiliki Wa nyumba Bila Hata Kuwa na nyumba

Hii ni Kupitia Uwekezaji ambao utanaweza Kukupitia Kipato Tulivu bila hata Wewe Kufanya kazi yeyote Ile
.
Na hapa nazungumzia Uwekezaji Wa halali kabisa na Siyo ponzi scheme kama vile LBL

Hapa nazungumzia Uwekezaji Kwenye sehemu halali kama vile.. Hatifungani

Na...

Mfano mzuri Wa Hatifungani Inayoweza kuanza kukupatia Kodi ni hii hatifungani ya Serikali ya Miaka 15 yenye riba ya 14.5% Ambayo itakuwa Kwenye mdana Wa wiki ijayo Tarehe 5
.
Kupitia Hatifungani hii Utakuwa ukipokea Kodi Yako (Riba) kama vile mwenye Nyumba BILA Hata Usumbufu Endapo Tu utawekeza Kwenye hatifungani hii
.
Ambapo...
.
Ukuwekeza kiasi cha Tsh. 10,000,000, basi Kodi yako itakuwa ikiingizwa Kwenye Account yako hivi:

Tarehe 06 Machi – Utapokea Tsh. 725,000 kwenye akaunti yako.

Na..

Tarehe 06 Septemba pia – Utapokea tena Tsh. 725,000.

Kwahiyo Kwa mwaka mzima, utakuwa umepokea Tsh. 1,450,000, na hiyo itadumu kwa miaka 15!

Na kama utawekeza Tsh. 50,000,000

Basi utapokea Kodi Yako kama ifuatavyo

Tarehe 06 Machi – Unatapokea Tsh. 3,625,000 kwenye akaunti yako.

Na...

Tarehe 06 Septemba – Utapokea tena Tsh. 3,625,000.

Kwa mwaka mzima, utapata Tsh. 7,250,000, na bado mtaji wako haujaguswa!

Labda utauliza..

Je, nitawezaje Kupokea Kodi (Riba) Kila Mwezi?

Okay Well, Utaweza Kupokea Kodi Yako Kwa kugawanya malipo yako kwa Kila mwezi

Ambapo ukiwekezaTsh.30,000,000, unapata Tsh. 2,175,000 Kwa kila baada ya miezi sita.

Hii inamaanisha Kwa Kila mwezi mmoja utakuwa ukipokea Tsh. 362,500 bila hata kufanya kazi yoyote!

Na ...

Hii Itakuwa kama vile mshahara wa mwezi Lakini tofauti wake ni kwamba, hapa huna bosi, huna wateja, Wala Huna wapangaji.

Na uzuri Wa Hapa ni Kwamba huhitaji Kuwa na kiwango chote hicho Ili Uweze kushiriki Kwenye Uwekezaji Wa Hatifungani hii ya miaka 15 kwani Kiwango cha chini kabisa cha kuwekeza ni Tsh. 1,000,000 tu!

Kwahiyo...

Hata Wewe Bado unayo nafasi ya kushiriki Kwenye Huu mdana Wa Hatifungani utakaofanyika wiki ijayo kwani Kila mtu anaruhusiwa kushiriki Kwenye Huu mdana

Na Incase unataka kushiriki Kwenye Huu mdana na unatamani Kufahamu Zaidi Jinsi ya kushiriki na kuweza kufaidika Zaidi na Uwekezaji Wa Hatifungani

Basi unaweza Kuanzia na hii Ebook Hapa Kwenye Link..Masoko ya Fedha na mitaji PDF

Hasta la Vista!

Habakuki Hussen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…