Zalisha funza, ni bonge la dili hapa mjini

Zalisha funza, ni bonge la dili hapa mjini

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
SOMO
UFUGAJI WA FUNZA


1716568467994.jpg


funza ni nini?

Funza hawa ni moja tu kati ya hatua za ukuaji za wadudu walukao, watu wengi hufikili hao funza hubaki kuwa funza mpaka mwisho jambo ambalo si la kweli hawa funza ni larval stage ya ukuaji wa wadudu ambapo wadudu hao wapepelukao hutua na kutaga mayai yao.

Wengine wanachukulia hawa wadudu ni uchafu na kinyaa ila FUNZA ni wadudu wenye PROTINI nyingi ambayo INAHITAJIKA sana kwa UKUAJI wa KUKU,SAMAKI,Nguruwe na mifugo mingine.

Utengenezaji wa Funza ktk kulisha mifugo hupunguza sana gharama za Chakula.

Zipo njia nyingi za Kutengeneza FUNZA.Ila NJIA RAHISI ni;Chukua Kinyesi cha Kuku/ng'ombe jaza kwenye dumu lililokatwa kisha weka pumba za mahindi kwa juu halafu nyunyuzia maji kidogo ili kuwavutia NZI waweze kutaga mayai hapo.Endelea kunyunyizia maji kwa siku 2 zaidi kisha acha.SIKU YA 4 FUNZA WATAANZA KUTOKEA,WAKUSANYE,WAOSHE NA KISHA WAPE KUKU WALE WAFAIDI.

Katika Nchi za wenzetu kuna Viwanda kabisa vya Kutengeneza FUNZA ambao hukaushwa na kuuzwa kwa nchi zingine.

Hii inaweza ikawa FURSA PIA hata Hapa Kwetu TANZANIA.Maana ni Rahisi na Soko lake ni Kubwa SANA.Na Ni kitendo cha Wiki Moja TU,unaanza Kula FAIDA za KUTENGENEZA FUNZA.
 
duu ukiwaza vile wanavyojazana alafu uanze kuwaosha tena 😶😶🤐 sema ndoivyo maokoto
 
Aaaah Chif Point kidogo to mpaka mtonyo Tz mnauwa reply text yangu inbox
Mbinu za masoko ni zilezile tu. Nikikupa simu uuze utafanyaje? Utakuja hapa kuuliza wapi nitapata wateja wa simu?
 
duu ukiwaza vile wanavyojazana alafu uanze kuwaosha tena 😶😶🤐 sema ndoivyo maokoto
Mchongo wa kutengeneza Pesa kwa mda Mdogo to kuliko kukaa mtaan hiii fursa afu simple Sana chakufanya kuwa tyr kufanya ah mbona kila k2 izy
 
Sasa kuna wadudu fulani weusi wako kama inzi lakini wao ni wakubwa nafikiri wanawaita inzi chuma sijui au black fly soulders hao wanatajwa kuwa na uwezo wa kuzalisha funza wengi sana kwa siku moja kuna jinsi ya kutengeneza namna ya kuwavutia ili waje kwenye taka ulizoandaa


Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Sasa mkuu kwani wakila bila kuwaosha itakuwaje?! Wataharisha?
 
Back
Top Bottom