Tatizo la nchi yetu bado ni lilelile la kwenda na ulimwengu wa Analogia wakati dunia iko Digitali.
Mi nadhani wizara ya uchukuzi ingeanzisha utaratibu wa Application au vipeperushi ambavyo vinakuwa vinaonyesha mikoa husika na aina ya ma-bus yanayoelekea huko.
Kwa mfano:
MKOA WA KILIMANJARO
LUXURY BUSES NA HUDUMA NDANI YA BUS
1.TILISHO - AC,WI-FI, etc.
2.BM - AC,WI-FI,VINYWAJI VYA AINA ZOTE.......etc
3.KIMBINYIKO -..........................
SEMI LUXURY BUSES
1.TILISHO - AC,HAKUNA WI-FI etc.
2.BM - WI-FI,HAKUNA AC WALA VINYWAJI
3.KIMBINYIKO - ....................
Huo ni mfano tu nimetolea na hivyo nisieleweke vibaya.
Sasa nadhani hii itaondoa ukakasi wa wale wapiga debe ambao huwa wanawajaza maneno mengi ya faraja abiria na ukiingia kwenye bus unakuta ni vice vesa,pia serikali kupitia wanaosimamia hayo ma-bus au usafirishaji abiria,unapoenda kukata tiketi kuwe kuna ulazima yule mkata tiketi akupe kitabu kitakachoonyesha aina ya bus na huduma zitolewazo na wewe unapaswa kulipia kile utakachokipenda.
Ili ukishalipa hiyo tiketi na ukapandishwa gari isiyokuwa na hizo huduma basi urudishiwe pesa yako na pesa ya kufidia muda wako.
Kinachotugharimu abiria wengi ni kwasababu hakuna mahali ambapo naweza kuona maelezo au taarifa zinazohusu hayo makampuni ya buses na huduma zitolewazo.
Kumbuka hakuna abiria anayependa kusafiri kwenda umbali wa kilometa nyingi kwa usumbufu na kero.
Taarifa ziwepo kuhusu hayo ma-bus na gharama husika ili kila abiria ajikadirie kwa uwezo wa mfuko wake,siyo nakuja stendi kukata tiketi nakuta bus limeandikwa ubavuni "luxury" na ukishapanda unakuta ni vice vesa.
Hebu tubadilike,tuache huu ubabaishaji wa kipumbavu.
Wao ngoja waendeleze huu ujinga na waendelee kuomba SGR isikamilike,lakini ikikamilika na ikafanya kazi kama tunavyoaminishwa,kiukweli ruti za ma-bus zitapungua,kwasababu siwezi kukaa kwenye bus kutoka Dar kwenda Mza kwa saa 17 wakati treni ni masaa 8 mpaka 10 tu.