Zama za Kilimanjaro Express zimeisha

Wapo hovyo sio uongo...
Hayo luxury nilipanda siku moja walisema iko na choo ndani kumbe ni haja ndogo tu... Sasa kuna mwanamke mmoja akafanya kubwa badala ya ndogo Aisee gari zima ilinuka safari ilikuwa chungu sana na watu walikuwa wanalalamika mno kuna harufu kali ndani..wakiwasha ac ni kama wanasambaza harufu tulikuwa tunasafiri kama tupo ndani ya choo tena ambacho hakiflash
 
Aisee uliichosema ni ukweli 100%. Nilikuwa nikisafiri Dar-Ars sipandi basi lingine tofauti na KLM. January nimesafiri na basi lao T 860 BVA limechoka mnooo, tangu hapo sina hamu na KLM tena.

Basi zina miaka 15 barabarani hiyo ni faida kwake, lakin kwa mimi abiria nipande ya nini wakati zipo Yutong na Zhongtong Upgrade mpyaaa

Sawaya abadilike kuendana na soko, watu wanashusha mchina wanatumia miaka 2 wanauza wanashusha mpya unakuta kampuni ina gari mpya kila siku mfno, Shabiby & BM. ila huyo jamaa anakomaa na zile APD, ASM, AXR, AWY miaka na miaka atleast zile G7 DHY & DMH
 
Achana kipengele cha AC nenda na hoja ya msingi, Dar maridi itoke wapi, wewe ulipokuja umetukuta tunatembea na makoti mchana kutwa kama huko.
Usiwe mkali basi jombaa🤣🤣🤣🤣 kwani umelipa shilingi ngapi? Kama ni 35k mi saivi haifiki sa6 nshaichoma kiberiti bar
Supu7k
Bia kumi Heineken 30k nyama choma au kuku nusu 9k kwa Dodoma
So tulia nextime panda BM
😅😅😅
 
Hapo mdau lazima atakuwa aliondoka na bus la saa 12 alfajiri, makampuni yenye mabasi mengi huweka magari ya zamani routes za alfajiri wakijua kabisa mteja huna option hasa kwa njia ambazo kuna gari kuanzia asubuhi mpaka mchana alafu za kuanzia saa 1 asubuhi na kuendelea ndio unakutana na michuma ya maana
 
Mkuu hakuna Luxury buses Tanzania kama wanavyozitaja.

Ni ile BM moja tu yenye seat nne mwanzoni za kuweza kuadjust na kulala comfortably na ina space ya kuweka food stuffs

Mengine yote ni matangazo tu...Mara Luxury, Mara semi luxury....hamna kitu.
 
Ngorika lipo siku hizi. Nakumbuka safari ya Kwanza toka dar to Moshi nilipanda basi linaitwa MBAZI sijui. Kwa kweli nilijuuuuuuuuuta, ndani gari ni siti 3 Kwa 2 afu ni zinabana miguu kama mtu ni mrefu nilijikuta nimekaa kupande toka dar mpaka nashuka moshi Kwa kweli nilijuta sana lile gari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…