Zama za mizaha ya Uhaini, Ugaidi na Uchochezi zifike mwisho!

Zama za mizaha ya Uhaini, Ugaidi na Uchochezi zifike mwisho!

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
790
Reaction score
1,316
Katika injili ya Luka 14:28-30, twasoma; "Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia? Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki, wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza"

Sina hakika kama wenye mamlaka wameshawahi kufanya tathimini ya kina, kama tangu tulipoingia kwenye mfumo wa vyama vingi, kesi zote za uhaini, ugaidi na uchochezi zilizowahi kufunguliwa, zimeleta tija yoyote kwenye nchi yetu.

Kwakumbukumbu zangu, kesi zote za namna hii, toka zianze kufunguliwa, washitakiwa huwa ni wanachama wa vyama vya upinzani na wanaharakati, walalamikaji huwa ni jeshi la polisi, na hizi kesi huisha kwa mwendesha mashtaka wa serikali kufuta mashtaka (nolle prosequi) au serikali kushindwa kesi.

Kama nchi hatuwezi kukubali kuwa kambi la magaidi, wahaini wala wachochezi. Watu wa namna hii kama wapo, basi ni wajibu wa vyombo vyetu kuwachukulia hatua. Hata hivyo tuwe wakweli kwa nafsi zetu; Je, huwa tunafanya tathmini ya kina kabla ya kuwakamata na kuwafungulia watu hii mikesi? Kama jibu ni ndio, kwanini hii mikesi ikishafunguliwa huwa inaishia kuyeyuka au serikali kushindwa?

Wilfred Lwakatare tuliambiwa ni gaidi, Jaji Lawrence Kaduri akamwachia huru, Mbowe tuliambiwa ni gaidi sasa yupo mtaani. Masheikh wa uamsho tuliambiwa ni magaidi nao sasa wapo mtaani. Lissu tuliambiwa ni mhaini, leo ni siku ya 473 bado kesi haijaisha. Sasa tunaambiwa lecturer gaidi mara vijana wa CHASO magaidi! jamani!

Nadhani tunayo haja na hoja ya kujiuliza kuwa hizi zama za mizaha ya kufunguliana kesi za uhaini, ugaidi na uchochezi zitaendelea mpaka lini na kwa maslahi ya nani. Jambo hili ni vyema lifike mwisho maana linachafua sifa nzuri ya nchi yetu.
 
Hiyo siyo mizaha na kamwe haiwezi kuisha mpaka pale tutakapo kuwa tumefanikiwa kudai na kupata katiba mpya maana hizo ndiyo defence mechanism za kuwafanya waendelee kututia hofu
 
Kwanini unatumua neno tu.... kuonyesha kama huu ujinga unafanywa na watanzania wote? Unge-address kwa Samia ambaye ndiye chanzo ya haya yote na siyo watanzania wote. Au pengine ni wewe na Samia?
 
4. MASHARTI NA MUDA MAALUMU KUTOKA COMMONWEALTH CMG(The Ultimatum)

Kutokana na mapendekezo ya Mjumbe Maalum, CMAG imetoa maelekezo yenye ukomo wa muda (Time-bound actions) kwa Tanzania:

Ndani ya Siku 30: Kutatua suala la kushikiliwa kwa Tundu Lissu kupitia njia za kisiasa au kisheria, na kuwaachia wengine wote wanaoshikiliwa kwa kutumia haki zao kwa amani.

Ndani ya Siku 60: Kurejesha upatikanaji kamili wa mitandao ya kijamii na kuacha vitisho dhidi ya vyombo vya habari na watetezi wa uhuru wa kujieleza.

Ndani ya Siku 90: Kuitisha jukwaa shirikishi na la kuaminika la vyama vya siasa (likiongozwa na mwezeshaji huru) kujadili mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi, ushindani wa kisiasa, wafungwa, na uwajibikaji.

Bila Kuchelewa: Kuanza uchunguzi huru wa makosa ya jinai uliopendekezwa na Tume ya Uchunguzi, pamoja na fidia kwa wahanga.

MWISHO WA UBAYA NI AIBU.
 
Kuna kitu/scenario wanaziita bila ya wao kujua.

Kuna kiongozi mmoja kule Malawi hupenda kuvaa tai yenye bendera ndio huwa anapenda sana hizi ishu ya UGAIDI.
 
Hawa vilaza kuna kitu wanakitafuta. Baada ya kuona kesi zao za uchochezi haziwanufaishi, wameamua kwenda hatua nyingine mbele! Sasa wanahubiri uhaini na ugaidi ili kuwakomoa wakosoaji wao. Siku huo uhaini na ugaidi ukotokea kweli, wasimtafute mchawi.
 
Kwanini unatumua neno tu.... kuonyesha kama huu ujinga unafanywa na watanzania wote? Unge-address kwa Samia ambaye ndiye chanzo ya haya yote na siyo watanzania wote. Au pengine ni wewe na Samia?
Comrade haya mambo ni complex sana. Amini usiamini, yapo yanayofanyika ambayo hata namba moja hayajui na hajayatolea maelekezo. Sababu kubwa inayochangia haya ni "uchawa"

Wapo wengi tu wanaoumiza wengine wakidhani namba moja atawaona kuwa wanampigania awapandishe vyeo. Wapo wengine wanaweza kumshauri vibaya kwania ya kujipendekeza tu.

Hoja yangu ni kuwa hili tatizo ni kubwa na nimtambuka. Haliwezi kutatuliwa kwa jibu moja rahisi.
 
Comrade haya mambo ni complex sana. Amini usiamini, yapo yanayofanyika ambayo hata namba moja hayajui na hajayatolea maelekezo. Sababu kubwa inayochangia haya ni "uchawa"

Wapo wengi tu wanaoumiza wengine wakidhani namba moja atawaona kuwa wanampigania awapandishe vyeo. Wapo wengine wanaweza kumshauri vibaya kwania ya kujipendekeza tu.

Hoja yangu ni kuwa hili tatizo ni kubwa kubwa na nimtambuka. Haliwezi kutatuliwa kwa jibu moja rahisi.
Huu ujinga kawadanganye wajinga wenzako. Ule wakati wa kudanganyana kuwa rais anaangushwa na wasaidizi wake siyo wa karne hii tena. Ukiwa rais na ukaona mtu yeyote aliyechini yako amefanya uhuni ambao hukumtuma, unachukuwa hatua mara moja na tena unaeleza umma ili wajue na viongozi wengine wapate kujifunza.
 
Kwa jinsi uchawa ulivyoshamiri namna hii, kama huamini kuna watu wanafanya mambo ya namna hii ili kujipendekeza kwa Rais, basi una safari ndefu sana ya kwenda.
 
Hiyo siyo mizaha na kamwe haiwezi kuisha mpaka pale tutakapo kuwa tumefanikiwa kudai na kupata katiba mpya maana hizo ndiyo defence mechanism za kuwafanya waendelee kututia hofu
Kama Sheikh Mwaipopo anayemiliki jeshi la chui weusi wanaotahiri watu bila ganzi siyo gaidi, ila Dr. Kaijage, lecturer wa UDOM ni gaidi; usipoiita hii ni mizaha, tuambie utaiita ni nini?
 
Kama Sheikh Mwaipopo anayemiliki jeshi la chui weusi wanaotahiri watu bila ganzi siyo gaidi, ila Dr. Kaijage, lecturer wa UDOM ni gaidi; usipoiita hii ni mizaha, tuambie utaiita ni nini?
viongozi wa nchi hii hawana aibu hata kidogo.
Mwaipopo hakutakiwa kuwa uraiani muda huu maana yeye ndiye anatakiwa kuwepo magereza kwani anamiliki jeshi
 
Back
Top Bottom