Zama zetu kali. Unakijua hiko kidubwasha wewee!?

Na shida ni hapo kwenye uzi maana magazeti utaokota tu hayo ya Komesha, Kasheshe na Alasiri sasa mtihani ni uzi.

Kuna baadhi ya fukwe naona wana vishada vya kishua
 
Na shida ni hapo kwenye uzi maana magazeti utaokota tu hayo ya Komesha, Kasheshe na Alasiri sasa mtihani ni uzi.

Kuna baadhi ya fukwe naona wana vishada vya kishua
Sisi tulikuwa tunatumia mifuko ya nylon ile malboro au mifuko ya mkate ila ya sankist
 
Huyu mbwa wa jirani anabweka kama anapiga vigeregere mi simkubali kabisa
 
Kumbe kaona ngedere. Hawa ngedere wamemaliza shamba la mahindi, mapera na naona wanavizia mafenesi. Ila hua naona ni bora wanavyopiga round kwa sababu nyoka watakua hawasogei.

 
Huu mchezo nimeucheza na kuna id hua zinajisema zina 40+ naona zinasema zimeucheza.

Nipo nashangaa hapa.
Siyo hizo tu hata nyingine zina 28- nazo zinasema zimeucheza yaani.
 
Huu mchezo nimeucheza na kuna id hua zinajisema zina 40+ naona zinasema zimeucheza.

Nipo nashangaa hapa.
40+ ndio watu pekee kutokea wenye akili kubwa zote na michezo yote wamecheza. Kuna Butua,wengine wanaita kombolela,kuna “mwakabunguja”,hii ndude unachukua viazi vitamu,unaviweka kiasi kama viazi 10,15 hivi unachimba shimo kidogo unazungushia mabonge ya udonge,unawasha moto huko ndani,unaziba,baada moto kuwa unaanza kupiga. Hiyo hasa huko kwenye kuchunga ng'ombe.Kwa tuliokulia Bush countries

kuna kujenge ghetto lako barabarani kwa home. Ile kipipindi cha sikukuu mnachangiana labda vijana kama wa5 hivi. Mnachagua ghetto la mmojawenu,mnatengeneza mzunguko wa lisasa,funga mziki wa kutosha,vyakula,makuku kuku n.k. Sikukuu kwenu murua kabisa.

kuna timu za kitaa za viniengo,kabumbu zilikuwa zinaundwa kulingana na eneo,umbali. Siku za week-end kuna viwanja tulikuwa tunakutana hapo,unakuta tumekutana hapo kundi la timu hata mpaka 6. Ilikuwa ni mpira wa kibabe sana,unakuta katikati ya mpira ngumi zinaibuka. Basi kamji kote kanazizima. Ole wako upigwe. Unafika home nako unakutana na fimbo kwa nini uonewe. Basi ilikuwa ni kujengewa ujasiri sana.


Hivyo vishada tumeunda sana,japo vyetu vilikuwa vya makaratasi ya nailon. Tengeneza sana magari ya udongo. Tengeneza sana magari ya mabox,na mambo mengine mengi. 40+ ndio tumefaidi maisha. Tumepitia mengi hatari.

Nashukuru sana yale malezi,ndio yamenifanya niwe imara sana,mvumilivu,mpambanaji,na mtafutaji sana. Sio nyie wa 1995 na kuendelea,hasa 2000 hapo mmekulia ndani tu kuangalia TV tu.
 
Hiko siyo kishada.

Kishada ni magazeti/ manailoni yanatengenezwa kufuatisha umbo la ndubwi kwa kutumia chelewa kisha unafungwa uzi unakiacha kipepee, huku ule uzi unautumia kuchagua kukiongeza urefu au kupunguza.
Sisi tulikua tunaita Tiara
 
Nimekimbiza sana hizi, tulikuwa tunatumia majani ya mikaratusi.
 
Halafu unachomeka msumari kama ‘detonator’, ikifika saa sita usikilu wa mwaka mpya mnazilipua 😂😂😂, wengine walitumia za pikioiki halafu wanachomeka bolt ndogo
Hahaa umesahau kupiga baruti tulikua tunatumia spoko za baiskeli halafu kule kwenye tundu unajaza ule unga wa njiti ya kiberiti
 
Helkopta unatakiwa ukimbie na upepo uwe mkali ili kizunguke[emoji3][emoji3]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…