40+ ndio watu pekee kutokea wenye akili kubwa zote na michezo yote wamecheza. Kuna Butua,wengine wanaita kombolela,kuna “mwakabunguja”,hii ndude unachukua viazi vitamu,unaviweka kiasi kama viazi 10,15 hivi unachimba shimo kidogo unazungushia mabonge ya udonge,unawasha moto huko ndani,unaziba,baada moto kuwa unaanza kupiga. Hiyo hasa huko kwenye kuchunga ng'ombe.Kwa tuliokulia Bush countries
kuna kujenge ghetto lako barabarani kwa home. Ile kipipindi cha sikukuu mnachangiana labda vijana kama wa5 hivi. Mnachagua ghetto la mmojawenu,mnatengeneza mzunguko wa lisasa,funga mziki wa kutosha,vyakula,makuku kuku n.k. Sikukuu kwenu murua kabisa.
kuna timu za kitaa za viniengo,kabumbu zilikuwa zinaundwa kulingana na eneo,umbali. Siku za week-end kuna viwanja tulikuwa tunakutana hapo,unakuta tumekutana hapo kundi la timu hata mpaka 6. Ilikuwa ni mpira wa kibabe sana,unakuta katikati ya mpira ngumi zinaibuka. Basi kamji kote kanazizima. Ole wako upigwe. Unafika home nako unakutana na fimbo kwa nini uonewe. Basi ilikuwa ni kujengewa ujasiri sana.
Hivyo vishada tumeunda sana,japo vyetu vilikuwa vya makaratasi ya nailon. Tengeneza sana magari ya udongo. Tengeneza sana magari ya mabox,na mambo mengine mengi. 40+ ndio tumefaidi maisha. Tumepitia mengi hatari.
Nashukuru sana yale malezi,ndio yamenifanya niwe imara sana,mvumilivu,mpambanaji,na mtafutaji sana. Sio nyie wa 1995 na kuendelea,hasa 2000 hapo mmekulia ndani tu kuangalia TV tu.