Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Nakumbuka enzi za Pius Msekwa, Sita na hata Makinda kidogo kulikuwa na mjadala mkali na mpambano wa fikra kuhusu qualities za mtu wa kushika Nafasi hii nyeti.
Ila Kwa miaka ya hivi Karibuni kiti Cha spika kimekuwa kama mchakato wa kumpata mwenyekiti wa Kijiji na siyo vijiji vyote.
Spika ameonekana kama katibu wa Chama, ameonekana kama mwenezi na wakati mwingine ameonekana kama kampeni meneji asiye na ukomo. Kiti Cha spika kimekuwa Mali ya yeyote atakayeonekana anafaa na Mwenyekiti wa Chama. Hakuna mjumbe anayeweza kutamka neno, hakuna wajumbe wanaoweza kuonyesha wanamuunga mkono nani Kati ya wachukua fomu, maana yake mwenye mamlaka ni mtu mmoja tu na huyo hakuna mwenye nguvu yakujadili wish yake.
Kwa mfumo huu hakuna spike Bali Kuna mwakilishi wa Chama kwenye Bunge. Kwa mfumo huu lazima anayeteua awe na mamlaka yakutengua, Kwa mfumo huu spika anakalia Kiti na kuendelea kukalia kiti pale TU mahusiano yake na Mwenyekiti yanapokuwa sawa . Wakikinzana wabunge wanategemea kupotishwa n mwenyekiti watamtoa Ili wapitishwe Tena.
VYOMBO vya habari vimejikiti kuripoti kinachotokea, havina mamlaka yakuchambua na kuonyesha wanaofaa, wao kazi Yao nikueleza kimetokea nn na hakuna kumkosoa mwenyekiti kwamba ameleta asiyefaa. Tuliona VYOMBO vya habari vikimsifia Ndugai kama Malaika, alipozingua tu vikaachana naye nakumpaka matope kama vile ni mpya kwenye uongoz kumbe alipoteza zamani dira ila tukamkalia kimya.
Tunakoelekea tutafika tumechoka Sana Kwa sababu tumeamua aliyepo sahihi siku zote ni mwenyekiti na atakosolewa pale TU atakapoachia kiti, vinginevyo hata afanye uovu vipi akiwa madarakani atutamsema Kwa sababu atatuma wasaidizi wake waje kutusaidia kujibeba