Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Hapo zama za kale niliamini kwamba unapoteuliwa kuwa msaidizi wa Mh. Rais basi wewe umepanda cheo na ni kiongozi mkubwa sana kwenye mfumo wa utumishi wa umma.
Mabadiliko yaliyowaondoa Ikulu akina Zuhura na Magoti sambamba na wengine wengi yamenifanya nibadili fikra kwenye hizi nafasi za umma.
Waliotenguliwa Ikulu wengi wamepewa nafasi ya ukuu wa Wilaya, DAS na RAS ambazo si nafasi za maamuzi makubwa au nafasi kubwa kwenye utumishi wa umma. Baadhi wamepewa ukatibu mkuu Msaidizi na wengine wamekwenda kupangiwa kazi maeneo mengine
Je, mfumo huu wa kutengua na kupangia watumishi wa umma unatengenezaje seniority? Kiongozi wa ngazi ya juu serikali ambaye hakuna namna yakumshushia hadhi ni nani?
Je wakuu wa vyombo vya usalama nao wakitumbuliwa hawawezi kupangia majukumu ya ukuu wa Wilaya, Mkoa, Karibu tawala na naibu KATIBU Mkuu? Je, kuna sheria au kanuni zinaroratibu hizi posts serikalini?