Zamani nilikuwa namshangaa mtu aliyefanikiwa kimaisha na hasaidii ndugu zake, Leo mimi natamani hata kuwapiga Risasi

Sio tu ndugu ila kwenye maisha hasa ya watu weusi aka WaAfrica jaribu sana kuwaweka watu mbali na wewe...uwe na urafiki wa kawaida tu na watu, haya mambo yakujifanya sijui rafiki yangu wa karibu na kujuana kiundani ni hatari, ndugu zako ni watoto zako na mkeo ( if she is good for you) wengine wote waweke mbali kidogo...
 
Lakini ukifa watakuzika tu utake usitake na watoto wako watatunzwa na wao.
Kwahiyo unachukua perceived future catastrophes kuji-hold hostage kwa hawa watu?

Its funny,maana na wao si watakufa like anybody else au wao wana tiketi ya kutokufa?

Kuzikwa is not an issue here....

Zote ni fear impacted by the society on you and u will never be free ukiwa hivi!
 
Na Kuna ndug wanakutafuta ukishapata kaz tu tena wengne hukuwahi hata kuwaona ukiwa mdogo mimi kwa sasa neno Sina siwezi kusema kwa wazazi tu ila hao wengine sahivi Kila siku jibu ni sina
 
Ndugu wana mambo ya ajabu sana..
Mimi wakati nipo mdogo nilikuwa namshangaa baba yangu kwa kuwakwepa ndugu zake nikamuona kama katili na ana roho mbaya..wakati nasoma hakuna alienisumbua kabisa..
Nilivyopata mahali pa kujishikiza tu.. nikafungua na kiduka mahali.. basi wanaona kama mimi mo sasa...
Kila siku matatizo yao tu.. mara mtoto anaumwa mara wao wanaumwa.. sa hv nimekubali dhambi tu..
 
Kweli kabisa
 
Nilijikuta nacheka hata kabla sijafungua thread yako. Ok ngoja niisome sasa
 
Kaa ukijua kuwa familia zenyewe hushindana
Yaani kila familia inataka iwe juu kuliko nyingine so unganisha nguvu za wadogo zako familia yenu iwe na nguvu wengine salamu tu inatosha
 
πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„ Undugu lawama.
 
Pole sana mkuu. Ungetuambia basi walikukosea nini sasa.....
 
huwajui tu ndugu

Hakuna wa kutunza watoto wako dunia ya leo, sana sana watagawana chako ulichokiacha. Hiyo ya kusema ndugu zako watakutunzia watoto wako ukifa inachekesha. Tumeshayaona mengi sana hapo siwezi kushawishika kukuelewa.
 
Hivi ndugu ukimpa mfano 50k utamaliza shida zake.?

Jibu ni hapana, na wala hatokushukuru kiviiile atasema si 50k tu na atarudi tena baada ya muda mfupi... lakini ukiwapa ndugu 10 tayari hiyo ni 500k ila wao hawajui wanaona 50k tu.

Siku ummyime sasa, we mnyime tu utaona!

Haya maisha tusaidiane kwa mawazo tu, haya hayana hasara... kwa pesa na vitu labda kwa nyakati za lazima tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…