Hili ndo tatizo kubwa... hafahamu kwamba Profit is a function of Total Revenue and Total Cost! Revenue ikiwa constant na ukakata/ukapunguza gharama za uzalishaji, profit inaongezeka... likewise, cost ikiwa constant na mapato yakaongezeka, profit pia hupanda. Mapato yanaongezeka ama kwa kuongeza bei au kuongeza mauzo... always it's bad idea kuongeza mapato kwa kuongeza bei especially kama kuna close substitutes... na haya ma-DSTv, Zuku, Startimes & Co, ni close substitutes coz' kote huko kuna movie za kibongo; so the best way to increase revenues is through increasing sales... mauzo yanaongezeka kwa ku-cut down price huku ukiongeza unit production! Mambo kama haya Zamaradi hawezi kuyaelewa kwahiyo tusimlaumu...
Lakini tukija kwa upande mwingine, Zamaradi na wenzake wana kila sababu ya kulalamika! Unaposhusha bei kuna two direct effects, mosi ni hiyo ya kujiongezea mauzo but second, ni ku-cut down competition! Si kweli hata kidogo kwamba watakaoathirika na pirates coz' hawa wezi wa kazi za wasanii hawanaa production costs kubwa... all they need to have is just PC a with multiple burners, Disk Printer, a bunch of low quality empty CDs ambazo huuzwa sh. 100/- and cartridges... that's it... kwahiyo hawa hata wakiuza kwa sh. 500/- bado hawapati hasara coz' they don't have movie production cost ambayo akina Zamaradi wanayo! Jibu sahihi ni kwa akina Zamaradi nao kuongeza mauzo through price cut kama walivyofanya Steps lakini suala la kuongeza mauzo nalo is directly related to your distribution channels... hili la distribution channels ndilo litakalokutofautisha wewe na mtu kama Bakhresa endapo leo utaamua kuanzisha a milling business manake unaweza kujikuta unashindwa kusambaza even within Kinondoni wakati mwenzako anafika hadi Kanyigo!