brenda18
JF-Expert Member
- Sep 17, 2013
- 5,687
- 5,287
Mke wa mtu pia anatogonzwa wanaume wanajisahau akishaoa anajua game over, uwiii mambo yamebadilikaHahahaha sema wewe.... watoaji mimba siku hizi ni wengi, hapo kwenye kuacha tupo sawa....
Hata tuoane kwa style ipi tufike ndani ya ndoa uniletee figisu najikata mapema.
Wanawake wengine kama wamelogwa familia unalea wewe, mume malaya na kipondo unapokea cha maana ila mkiwa machoni pa watu fake faces mpaka basi na bado tu mtu kakomaa kama aliambiwa akiondoka anakufa.
Ndoa ni zaidi ya tuvionavyo na maisha ni kuishi na kuchagua
Kiukweli ndoa za zamani zilidumu kwasababu mama zetu walijikaza sana kuhakikisha hawatengani
Ila karne hii ili mahusiano yadumu unahitaji pande zote mbili zijitoe haswaa, huo ndio ukweli
Ila wanaume bado utawasikia wanawake wa siku hizi si wavumilivu, khee umeshasema wa siku hizi cope with it
Kama mwanaume hayupo tayari kutulia aisee bora asioe tu