screpa
JF-Expert Member
- Sep 10, 2015
- 10,857
- 15,866
Huyu mtangazaji wa Clouds TV, Sielewi hawa watu anaowahoji lengo lake ni nini, naona upumbavu anaoongea Gigy Money kwenye kipindi chake cha Take One, najiuliza kwanini anaruhusu ujinga huu. Nilidhani amejifunza na ile ishu ya yule shoga kumbe bure kabisa
Show ya zamaradi leo haina maadili kabisa ni afadhali ya yule shoga kuliko huyu malaya Gigy money
Interview zake na sijui zinafundisha nin jamii
Nitashangaa TCRA kukaa kimya baada ya hii show
=========
Gigy Money Jumanne hii aliwaacha mdomo wazi mashabiki wake baada ya kuwataja live kwenye runinga mastaa 6 wakiume aliotoka nao kimapenzi.
Video queen huyo ambaye amewai kutamba katika video za mastaa mbalimbali wa bongo, amedai amewai kutoka kimapenzi na AliKiba, Abdu Kiba, Rich Mavoko, Harmonize, Hemed Phd pamoja na mtangazaji wa kipindi cha runinga cha Siz Kitaa cha Clouds TV, Castro Dickson ambaye alidai alikuwa tayari kumzalia mtoto.
“Nilikuwa na Castro mpaka nilikuwa tayari kumzalia,”
Gigy Money alikiambia kipindi cha Take One cha Clouds TV.
“Kwa sababu anajua upendo kwa mtoto, lakini wakaja wanawake wamjini wakakorofisha, lakini hajawai kuniambia kama tumeachana, sijui kama tumeachana,”Gigy ambaye pia ni mtangazaji wa Choice FM alidai Mama yake mzazi alimzaa nyuma ya mlango wa choo.
Pia alisema kwamba aliwahi kujitoa kimwili katika umri mdogo ili apate hela ya kuweza kumnusuru mama yake mzazi kulipa deni la mkopo wa Benki.