Mr Bean.
Senior Member
- Jan 25, 2015
- 185
- 128
Katika hali isiyoyakawaida Zamaradi Mketema mtangazaji wa Clouds Tv leo hii amemualika mdada mmoja anajiita Gigy Money Ambae nae pia ni mtangazaji wa hizi Radio za FM. Huyo dada bila aibu anaelezea bila kuficha mambo yake ya ajabuajabu na anaelezea watu aliowahi kutembea nao kwa kuwataja kwa majina Kawataja mastaa kadhaa wa bongo akiwemo Alli kiba na mdogo wake. Hemedi anaejiita PHD nawengineo Kinachonishangaza ni jinsi huyo Zamaradi alivyo na ujasiri wa kuandaa kipindi hili ikiwa ni wiki kadhaa tu zimepita alilaumiwa kwa kumualika shoga ktk kipindi chake cha takeone. Kwa kweli ni aibu kama ulikuwa upo unaangalia tv na watu unaowaheshimu ni balaa tupu. Ivi hawa TCRA wapo kweli.