Zamaradi Mketema aomboleza msiba wa ghafla wa paka wake baada ya kushambuliwa na mbwa

Zamaradi Mketema aomboleza msiba wa ghafla wa paka wake baada ya kushambuliwa na mbwa

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Kwa uchungu mzito Zamaradi Mketema aomboleza msiba wa ghafla wa paka wake baada ya kushambuliwa na mbwa

"Sijawahi kutegemea kama nitaumia hivi kwa kiumbe tofauti na mwanadamu, Paka wangu anaitwa HANNA, usiku sijui kitu gani kimemtuma atoke nje, kametokea dirishani akakutana na mbwa maana mbwa huwa tunawafungulia usiku tu wakamuumiza mno, na hii ni mara ya pili

mara ya kwanza alitokaga mbwa wakamshambulia bahati nzuri tuliwawahi akawa hoi lakini akapona kabisa akawa sawa, na akawa muoga kutoka ndani usiku sasa sijui kajisahau nini jamani katoka tena kilichomkuta this time hajapona,

nimeumiaaaaa 😭😭😭😭 Kalikuwa karafiki kazuri sana, nikirudi tu nyumbani lazima anikimbilie, na kila ninapoenda anakuwa nyuma!! Na utakapokaa lazima kawe pembeni, na kuna muda kachokozi kwelikweli lakini ni usumbufu wenye raha ndani yake, Dah!! Nimeumia kwakweli" - ameandika

Source: Swahili world on Facebook
1725376107609.jpg
 
Watu wengi wanaofuga paka,mbwa huwa wana bond nao sana.
Hii kama haijakutokea huwezi elewa kabisa,huko way back home tulikuwa na kapaka kazuri sana,kakaanza.kuelewa baadhi ya mambo tuliyo kafundisha ,binafsi nilikapenda sana,kuna dogo ndugu yetu mtundu akaja kukasokomeza na ufagio wa chelewa sehemu ya utupu wa nyuma na kalikuwa kadogo

Dah kalikuja kufa,aisee nilipata simanzi sana,kwahiyo namuelewa sana zamaradi,yaan ningekuwa karibu nae ningempa hug la maana sana kumfariji
 
Back
Top Bottom