Zamaradi wa Clouds Media ni binti shujaa

Stream line

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2015
Posts
393
Reaction score
239
Siku zimepita toka nijionee kipindi kimoja chenye mada ya ushoga. Mrushaji alikuwa zamaladi. Nilimwona siku hiyo na sijawahi kufuatilia vipindi vyake. Baadaye nilisikia viongozi wa TCRA wakiiadhibu clouds tv (tv ya vijana).

Hivi majuzi nimesoma magazeti serikali imepiga marufuku NGO zinazoshughulika na ukimwi, baada ya kugundua madudu wanayoyafanya ktk suala la ushoga. Pia nilisikia pale muhimbili serikali ilichukua hatua kama hiyo baada ya Zamaladi kurusha hewani kipindi hicho - sikujui jina.

MAONI YANGU:
Bila zamaladi NGO hizi zingendelea kufanya hayo.
TCRA msifanye kazi kwa kujitoa akili, hili jambo ni jepesi sana. Msiwe na mazoea ya kuwakatisha waandishi wa habari kama wamejitolea kutuhabarisha yaliyo ya halisi ktk jamii.

Kijana yule wa zamaladi aliiongelea hali halisi. Toka malezi hadi kujitegemea. Kumdhalilisha zamaladi ni sawa na kuzipinga juhudi za kuwasaida watu kama kijana yule.

USHAURI: TCRA iombe radhi clouds tv kwani kwa kutumia tv hiyo leo serikali imegundua hizo NGO na kufikia kuzifuta. Zamaladi uwasamehe TRCA (hawa wana ujuzi wa kutumia mabilioni kwenye vikao) kwani kwa kutumia evidences za NGOz kufungiwa clouds inaweza kufikisha kesi ya madai na udharirishwaji wa Zamaladi.

MWISHO: hongera zamaladi mama shujaa. Umeweza kusaidia kupunguza tatizo la ushoga. Aliyekusikiliza hasa the mamaz wameelimika juu ya kutunza watoto wao.

Asante.
 
Nimemwita binti kutegemea umri wangu. Hapa naongelea kijana shoga. Je, ina maana hicho kipindi siku hizi hakipo? Kipindi hicho ni kizuri sana. Mama zamaladi kama talent yako inaleta taabu hapa TZ tafutanchi za nje you will be great.
 
Kwa maana hiyo wewe unaweza kuwa mama wa Zamaradi kiumri?

Sasa kwa nini unapenda vipindi vya mashoga, je una watoto wako mashoga?

Hivi pale alikuwa anatangaza ushoga au anapunguza ushoga?

Hivi mtu kuhoji mashoga tayari anakuwa Na talent ya utangazaji?
 
kwa huyo kumuonesha yule shoga na kumhoji ni ushujaa, "industral revolution" naiona,
 
Kinachowapeleka nyumba za ibada nini? Je si kuyakemea maovu? Yesu alisema....aanze kumpiga mawe. Je, ni vibaya kijana huyo kujitangaza na kulilia msaaada mkubwa wa kisaikologia? Kama zama alifanya makosa je, ni wangapi wameokolewa kufuatia kipindi chake? Je, ni kwa nini Afya wazifunge NGOz? Kwani Afya haipo siku zote? Je, hawakuwa nao humo muhimbili? Zama kwa jamii yetu atabaki kuitwa Shujaa. Tena wa kweli.
Kwa kujitoa akili sasa makanisa yanafungisha ndoa za jinsia moja. Hata wachungaji nao wanaoana wa jinsia moja. Bila kuwatafuta vijana kama huyu wa Zamaladi tatizo hatutalimaliza.
 
Siku zimepita toka nijionee kipindi kimoja chenye mada ya ushoga. Mrushaji alikuwa zamaladi. Nilimwona siku hiyo na sijawahi kufuatilia vipindi vyake. Baadaye nilisikia viongozi wa TCRA wakiiadhibu clouds tv (tv ya vijana).

Hivi majuzi nimesoma magazeti serikali imepiga marufuku NGO zinazoshughulika na ukimwi, baada ya kugundua madudu wanayoyafanya ktk suala la ushoga. Pia nilisikia pale muhimbili serikali ilichukua hatua kama hiyo baada ya Zamaladi kurusha hewani kipindi hicho - sikujui jina.

MAONI YANGU:
Bila zamaladi NGO hizi zingendelea kufanya hayo.
TCRA msifanye kazi kwa kujitoa akili, hili jambo ni jepesi sana. Msiwe na mazoea ya kuwakatisha waandishi wa habari kama wamejitolea kutuhabarisha yaliyo ya halisi ktk jamii.

Kijana yule wa zamaladi aliiongelea hali halisi. Toka malezi hadi kujitegemea. Kumdhalilisha zamaladi ni sawa na kuzipinga juhudi za kuwasaida watu kama kijana yule.

USHAURI: TCRA iombe radhi clouds tv kwani kwa kutumia tv hiyo leo serikali imegundua hizo NGO na kufikia kuzifuta. Zamaladi uwasamehe TRCA (hawa wana ujuzi wa kutumia mabilioni kwenye vikao) kwani kwa kutumia evidences za NGOz kufungiwa clouds inaweza kufikisha kesi ya madai na udharirishwaji wa Zamaladi.

MWISHO: hongera zamaladi mama shujaa. Umeweza kusaidia kupunguza tatizo la ushoga. Aliyekusikiliza hasa the mamaz wameelimika juu ya kutunza watoto wao.

Asante.
Clouds FM and TV inaongozwa na watu wenye IQ ndogo sana,...sema Vijana tumekosa mbadala WA media ..efm nao bado hawakidhi haja ya Vijana... Hii thread imeandikwa na mtangazaji WA clouds namfahamu..!! Nasema tena nyie mmekosa substitute goods but your days are numbered
 
Siku zimepita toka nijionee kipindi kimoja chenye mada ya ushoga. Mrushaji alikuwa zamaladi. Nilimwona siku hiyo na sijawahi kufuatilia vipindi vyake. Baadaye nilisikia viongozi wa TCRA wakiiadhibu clouds tv (tv ya vijana).

Hivi majuzi nimesoma magazeti serikali imepiga marufuku NGO zinazoshughulika na ukimwi, baada ya kugundua madudu wanayoyafanya ktk suala la ushoga. Pia nilisikia pale muhimbili serikali ilichukua hatua kama hiyo baada ya Zamaladi kurusha hewani kipindi hicho - sikujui jina.

MAONI YANGU:
Bila zamaladi NGO hizi zingendelea kufanya hayo.
TCRA msifanye kazi kwa kujitoa akili, hili jambo ni jepesi sana. Msiwe na mazoea ya kuwakatisha waandishi wa habari kama wamejitolea kutuhabarisha yaliyo ya halisi ktk jamii.

Kijana yule wa zamaladi aliiongelea hali halisi. Toka malezi hadi kujitegemea. Kumdhalilisha zamaladi ni sawa na kuzipinga juhudi za kuwasaida watu kama kijana yule.

USHAURI: TCRA iombe radhi clouds tv kwani kwa kutumia tv hiyo leo serikali imegundua hizo NGO na kufikia kuzifuta. Zamaladi uwasamehe TRCA (hawa wana ujuzi wa kutumia mabilioni kwenye vikao) kwani kwa kutumia evidences za NGOz kufungiwa clouds inaweza kufikisha kesi ya madai na udharirishwaji wa Zamaladi.

MWISHO: hongera zamaladi mama shujaa. Umeweza kusaidia kupunguza tatizo la ushoga. Aliyekusikiliza hasa the mamaz wameelimika juu ya kutunza watoto wao.

Asante.
Lazma wewe uliendika ni mtu wa clouds fm maana akili zenu zote ziko sawa.
Basi iko Hivi, ili TCRA waweze kufanya maamuzi kama moderators wa media lazima kuwa na malalamiko claims kutoka kwa watumiaji wa media au waangaliaji, wanazipokea wanazifanyia uchunguzi alafu wana fanya maamuzi, hii inamaanisha hawafanya maamuzi hayo wao wenywe basata. Maamuzi haya hutokana na msukumo wa general public, ndio mana watu walikuwa wanawabeza wengi kwanini wasifungie kipindi, iliwachukua muda kukusanya malalamiko na kufanya uchunguzi, nadhani walifanya hivyo kwa kipindi chenu kingine clouds kinaitwa bibi bomba nacho ilikuwa ivyo ivyo wanapokea malalamiko wanafuatilia kwa kufanya uchunguzi kisha wanafanya maamuzi kutokana na malalimiko hayo kama communication regulators, leo hii wewe ukisema Zamaradi ameonewa na TCRA ni uongo, lazima utakuwa mtangazaji unasema hivyo, au mtoto mdogo maaan hata bosi wao anaelewa mchakato wa kufunga kipindi, kabla ya kufunga hiko kipindi nilipata piga stori na kamati ya maadhui ya TCRA nao wakakiri kupokea malalamiko mengi kutoka kwa watu tofauti juu ya kipindi, sasa ni hivi, vipindi vyote vya media lazima vifuate mueleleo sahihi kutokana na guidelines za tcra na mct usipokidhi hivi viwango wana kila haki ya kukifunga! Na pia, zingatia yule dada hakumhoji huyo shoga kisahihi, yani alifanya one sided interview ambayo haikuwa balanced. umeshawahi ona interview za cnn mkuu? unahojiwa wewe baba yako mama yako mwanafamilia, mwanajamii daktari na mwanasaikolojia, yaani kila mtu ambae anaguswa na hiyo mada anahojiwa na mnaoneshwa negative na positive effects, kama hujanielewa angalia interviews za oprah winfrey. Kamwe haiti mtu mmoja alafu kumhoji kuhusu sensitive issues bila kuonesha positive negative effects pamoja na angle zote za izo issue. Sasa wewe usiosomea Media utaon sawa kulishwa makapi kama hayo ila mtu mwenye akili hawezi angalia interview za shoga kuhojiwa kujidai kabisa ushoga unamuingizia hela, hiyo interview inasaidia nini??? inamsaidia nani? Na yule shoga angethubutu kutaja wateja wake kama alivyokuwa anaambiwa wangepelekwa mahakamani sio tu kufungiwa.
 
Back
Top Bottom