Lunyungu, good to see you back.
Namuunga Zambi mkono in principal kwamba wale wote waliosomeshwa na serikali huku nje warudi kuitumikia Taifa japo kwa muda fulani kama kurudisha fadhila and offcourse kujenga nchi. Sioni kama ni matumizi makini ya kodi za wananchi iwapo hela zinatumika kusomesha wananchi nje halafu hawarudi kuwatumikia wananchi waliowasomesha.
Sasa tunaweza kujadili iwapo kubaki nje ya nchi kunaweza kuongeza uzalishaji Tanzania kwa namna moja au nyingine.
Katika kuonyesha kujisafisha na lawama za kuiba wasomi waliosomeshwa na Serikali zao; waingereza wakaja na utaratibu kuwa iwapo umesomeshwa na Serikali au British Council ni lazima wakupe barua ya kukuruhusu kufanya kazi UK kabla hawajakubalia kukupa Work Permit. Sasa kwa kiasi fulani naona iwapo hii itafuatiliwa na makini kuliko ilivyo sasa inaweza kurudisha kodi za wananchi japo kidogo.
Ukiwa mwingereza ukaenda kufanya kazi nje, sehemu ya mshahara wako inaingia kwenye serikali yako. Kwa maana ya kwamba haijalishi upo wapi, ili mradi unazalisha kipato pale ulipo basi serikali/ wananchi wako inafaidika moja kwa moja.
Watu aina ya Lunyungu na Mwanakijiji......Mkuu ngoja watu waseme wenyewe acha kupiga mayowe!!!Leo mapema nikiwa ndani ya ukumbi wa Bunge , ndugu Zambi alisimama kuchangia na akataka kujua kwa nini Serikali isitumie nguvu kuwarudisha nyumbani ma expert wote watanzania wanaofanya kazi nje ya Nchi na kupata kipato kikubwa .Haya yalizuka baada ya Bunge kuelezwa kwamba watu wakisha soma Ulaya hubakia na kupata mishahara minono huko .
Kombani kasimama na kusema serikali inaweza kusema nasi kwa utaratibu wa kutuomba na si kuomba kwa nguvu tunyimwa ajira .Huyu Zambi nimeshangaa uwezo wake wa kuelewa mambo .Mwaka 2008 yeye anafikiria miaka ya 60 ? Wewe unasemaje ?
Leo mapema nikiwa ndani ya ukumbi wa Bunge , ndugu Zambi alisimama kuchangia na akataka kujua kwa nini Serikali isitumie nguvu kuwarudisha nyumbani ma expert wote watanzania wanaofanya kazi nje ya Nchi na kupata kipato kikubwa .Haya yalizuka baada ya Bunge kuelezwa kwamba watu wakisha soma Ulaya hubakia na kupata mishahara minono huko .
Kombani kasimama na kusema serikali inaweza kusema nasi kwa utaratibu wa kutuomba na si kuomba kwa nguvu tunyimwa ajira .Huyu Zambi nimeshangaa uwezo wake wa kuelewa mambo .Mwaka 2008 yeye anafikiria miaka ya 60 ? Wewe unasemaje ?
Kitu ulicho ongea Yebo Yebo ni sawa, kama wewe ulisomeshwa kwa pesa za walipa kodo wa TZ kwanini usirudi nyumbani kufanya kazi? hiyo system ya UK kukusanya kodi wa wanaofanya nje ya UK pia inatumiwa na South Afrika. Hivyo kama mtu atataka kubaki mtoni basi ni wajibu alipe kodi kufidia gharama ya kumsomesha.
Pia Mh Zambi cjui atasema vipi kwa wale wapiga box wanao jisomesha wenye na si watoto wa MAFISADI?
Mnawasomesha wa nini wakati hamtaki kuwaajiri?
Ni muhimu kuchunguza kiini hasa cha experts hawa kubaki nje ya nchi...
Mhe hii ni dhana potofu ya kusema unasoma ili uje kuajiriwa. Inabidi tubadilike kwa haraka sana kama tunahamu ya maendeleo ya kweli.
ELIMU sio lazima uje kuajiriwa ndio unufaike nayo. Mimi naona ni muhimu serikali iendelee kusomesha wananchi wake kuanzia msingi mpaka chuo kikuu. China na mataifa mengine yaliyoendelea walifanya hivyo na leo wapo mbali.
Elimu kwanza hayo maswala ya ajira ni matokea, lakini ukiwa na elimu na ukaamua kuitumia vizuri hata ukiuza genge hautakuwa sawa na muuza genge mwenzako asiye na elimu.
Lunyungu
Hii habari ndivyo hivi ilivyosemwa na huyo mhe au umeipinda??
Iwapo alisema wale wote waliosomeshwa na serikali basi naona kuna ulazima wa kurudi au kuitumikia nchi kwa namna moja au nyingine.
Mkuu YeboYebo
Salaam toka Dodoma .Umeuliza kama ndivyo alivyosema Mkuu Zambi nami nasema nime translate maneno yake maana Zambi anajua kuwa Yebo yebo, Lunyungu , Mwanakijiji , Jasusi na wengine ndipo nikaamua kutoka nje na kuwatumia ujumbe huu .Zambi alijawa na jazba na alitaka kusema asikike kama yuko Bungeni , alionekana akiwa na huzuni maana anasahau kwamba sisi watoto walalahoi hatuwezi kupata kazi Ikulu , Usalama wa Taifa , BoT,TRA nk .Ndiyo maana sisi tumeamua kuingia mitini na hata baada ya kuitumikia Tanzania kwa moyo wangu wote .
Sasa hii ndiyo habari yenyewe toka Dodoma