Daily News; Friday,August 15, 2008 @20:10
Habari nyingine
Kesi ya Prof. Mahalu yaahirishwa
Salma Kikwete azungumzia vikwazo vya elimu
Soko huria lawabana wakulima pamba
Milioni 278/- kutengeneza barabara za Mkinga
NSSF kujenga maghorofa 60 ya askari
Reli ya kaskazini yaanza kutumika
D.B Shapriya kutangazwa hafai
Watumishi 35 wa serikali wang'ang'ania nje
Watupwa jela miaka 30 kwa ujambazi
DC Tabora awashangaa wanaoibeza serikali
Watumishi 35 waliofadhiliwa mafunzo katika nchi mbalimbali duniani zikiwamo Uganda, Afrika Kusini, Uingereza na Marekani kati ya mwaka 1998 na 2008, hawakurejea nchini, Bunge limeelezwa.Watumishi hao na idadi yao katika mabano ni wauguzi waandamizi (17), wahadhiri fani ya uhandisi watatu, walimu wa lugha, wahadhiri fani ya ualimu, wataalamu wa teknolojia ya habari na ofisa tawala wote wawili kila fani.
Wengine ni Mtaalamu wa Jiolojia, Mchumi, Mtaalamu wa Takwimu, Mtaalamu wa Mazingira, Katibu Mahsusi na Mpishi Makazi ya Viongozi.Akijibu swali kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Celina Kombani alizitaja hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kuwaachisha kazi na juhudi za kuwafuatilia wengine zinaendelea ili kutambua kama wapo kwa kuwa taarifa rasmi ya wao kutorejea nchini hazijapatikana.
Katika swali lake, Mbunge wa Mfenesini, Mossy Suleiman Mussa (CCM), alitaka kauli ya serikali kuhusu hasara ya kuwasomesha watumishi wake nje kwa kuwa mara wamalizapo masomo hawarejei.Pia alitaka kujua ni hasara kiasi gani imepatikana tangu mwaka 1998 hadi 2008 kutokana na watumishi hao kutorudi nchini.
Akijibu hoja hizo, Kombani alikiri kuwa ni kweli nchi inapata hasara. Alisema wako watumishi waliopelekwa masomoni nje ya nchi kupitia wizara na taasisi mbalimbali za serikali ambao hawakurudi nchini kutoa huduma inayotokana na mafunzo hayo.
Aidha, alisema wabunge kuacha taaluma zao na kuingia kwenye siasa inawezekana ni kufuata maslahi mazuri ama kuwawakilisha wananchi.
Alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi (CCM). Katika swali lake la nyongeza, Zambi alihoji juu ya watumishi wa serikali wanaopelekwa masomoni nje ya nchi kutorejea baada ya kumaliza na kwa nini serikali isiziandikie barua nchi husika kutowaajiri.
Kombani alisema kuwabana sio vizuri labda wanatafuta maslahi kama baadhi ya wabunge walivyoacha taaluma zao na kuingia kwenye siasa."Kuwabana sio vizuri, huenda wanaangalia maslahi mazuri, hata baadhi ya wabunge wameacha taaluma zao na kuanza siasa labda ni maslahi au uwakilishi wa wananchi," alisema Kombani.