Icadon
JF-Expert Member
- Mar 21, 2007
- 3,581
- 193
Leo mapema nikiwa ndani ya ukumbi wa Bunge , ndugu Zambi alisimama kuchangia na akataka kujua kwa nini Serikali isitumie nguvu kuwarudisha nyumbani ma expert wote watanzania wanaofanya kazi nje ya Nchi na kupata kipato kikubwa .Haya yalizuka baada ya Bunge kuelezwa kwamba watu wakisha soma Ulaya hubakia na kupata mishahara minono huko .
Kombani kasimama na kusema serikali inaweza kusema nasi kwa utaratibu wa kutuomba na si kuomba kwa nguvu tunyimwa ajira .Huyu Zambi nimeshangaa uwezo wake wa kuelewa mambo .Mwaka 2008 yeye anafikiria miaka ya 60 ? Wewe unasemaje ?
Alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi (CCM). Katika swali lake la nyongeza, Zambi alihoji juu ya watumishi wa serikali wanaopelekwa masomoni nje ya nchi kutorejea baada ya kumaliza na kwa nini serikali isiziandikie barua nchi husika kutowaajiri.
No Comments
Source