Zambia kuzuia Mahindi kuingia Tanzania ni kutowapenda Wakulima Wake?

Mambo huwa hayaendi hivyo, hizo kauli za kudai "mkulima aruhusiwe kuuza chakula popote" ni za kisiasa na haziwezi kupata nafasi kwenye nchi ambazo wapo makini na uchumu wake.

Regulations ni lazima ziwepo.
Regulations za kuwaonea wakulima manamba wa watu wa mijini ?? Au ?? Mkulima anaweza akaja mjini akapanga bei ya kununua dawa kwa ajili ya familia yake ??!!
 
Njaa mnajitakia wenyewe, kulima hamtaki, ardhi ipo ya kutosha. Wengine wakilima muwapangie bei how? Mnajua ametumia gharama kiasi gani? Mwache auze ambako anaona atarudisha pesa aliyowekeza.
Sio sahihi kuruhusu wageni waende moja kwa moja vijijini kwa wakulima kununua chakula huko ni kutengeneza uhaba na ongezeko la bei.

Binadamu wana mgawanyiko wa majukumu Haiwezekani wote tukafanya shughuli moja hivyo hiyo hoja yako ya kusema ukitaka bei ndogo ya mazao ukalime hayo ni majibu mepesi kwa mtu asiyefikiri sawa sawa.
 
Nachokataa ni kunipangia bei na mahali pa kuuza wakati hujui gharama kiasi gani nimetumia, na bei unayonipangia gharama zangu zitarudi ama la. Anayetetea kupangiwa bei ya kuuza mazao na serikali huyo sio mkulima. Akalime na yeye kama anadhani kulima ni rahisi
Kilimo Cha Sasa hivi ni biashara sio UTI WA MGONGO
 
Hii nchi ina upuuzi mwingi sana
 
Tafuta shamba ukalime ujue uchungu wa kulima.
 
Shida nini si Ina motivated
Hata wakulima wa KAHAWA kule Kagera wanaruhusiwa kuuza uganda?
Wanafanyiwa hujuma tu wao ndio wanaotoka jasho.
Pana mijitu inanufaika kwa jasho lao tu
 
Mambo huwa hayaendi hivyo, hizo kauli za kudai "mkulima aruhusiwe kuuza chakula popote" ni za kisiasa na haziwezi kupata nafasi kwenye nchi ambazo wapo makini na uchumu wake.

Regulations ni lazima ziwepo.
Tunataka mkulima anufaike kupitia kazi yake ili kupunguza idadi ya machinga na bodaboda mijini.
Kwani hizo Sio kazi na haziwezi Inua uchumi,kilimo kikilipa watarejea vijijini kulima na kupunguza population mijini.
Sio kutwa nzima mtu anazurura mtaani anauza soksi au tai moja tu haya ni matumizi mabaya ya nguvu kazi nchini.
Kilimo kikilipa waote watarejea shamba wakabomoe visiki
 
Kwa hiyo zambia wameamua kokomaa wakenya wasipate mahindi, kama wametoa vibali kwa nini wayazuie?
Nazani ni wakati wa Kaunda au Chiluba,kuna kipindi ungaa wa ugali ulipanda bei kidogo tu, wananchi hao barabarani wamegoma, hadi unga ukashuwa bei na kurudi bei ya zamani hapohapo!!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Rais keshapewa chake,yeye akae pembeni watu wapige kazi!!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Serikali makini ununua mazao yote toka kwa mkulima then uyatunza na kuja kumuuzia Tena mkulima huyo huyo kwa Bei ya faida hapa inakuwa imepata faida kupitia mkulima na pia mkulima anakuwa na uhakika wa soko la mazao yake.Ndivyo walivyofanya wakoloni kazi ya mkulima ni kuwaza kubomoa mapori zaidi alime zaidi kazi ya soko ni ya Serikali
 
Mapori yamejaa hayana faida si wapewe wenye kumudu kulima walime wengine tupate ajira
 
Limeni wekeni stock ya kutosha ya kula mwaka mzima acheni kelele mitandaoni
 
We mrundi tulia la sivyo tutakupiga patresheni urudi kwenu bujumbura
 
Kiukweli kwa upuuzi unaoendelea Tanzania kuuza chakula kipuuzi namana hii..tutakuja kujuta mbeleni
 

Mkulima hana lolote analonufaika nalo kwenye utaratibu huo mpaka sasa, hizi ni propaganda za wafanyabiashara. Mkulima atabaki vilevile, kama ilivyo sasa.
 
Regulations za kuwaonea wakulima manamba wa watu wa mijini ?? Au ?? Mkulima anaweza akaja mjini akapanga bei ya kununua dawa kwa ajili ya familia yake ??!!

Hahaha, tatizo wengi mnayapeleka haya mambo kinadharia zaidi, ukweli ni kwamba bila kuweka regulations nzuri bado mkulima sio mufaika wa hizi taratibu zilizopo, ila ni wafanyabishara na itabaki kuwa hivyo siku zote.

Wakulima wananufaikaje ikiwa baada ya kuuza hayo mazao ndani ya miezi miwili tu tunaaza kuimba nao wimbo mmoja " chakula bei juu" ..?

Bado mkulima sio mnufaika na wala hatakuja kunufaika ikiwa utaratibu utabaki kuwa huu.
 
Mkulima hana lolote analonufaika nalo kwenye utaratibu huo mpaka sasa, hizi ni propaganda za wafanyabiashara. Mkulima atabaki vilevile, kama ilivyo sasa.
Hayo magari yanayozunguka mashambani je
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…