Zambia kuzuia Mahindi kuingia Tanzania ni kutowapenda Wakulima Wake?

nafanya biashara ya vyakula na nafaka natoa tanzania kwenda zambia na malawi , natoa malawi na zambi kuleta tanzania kutegemea na msimu na soko linataka nini, nikufundishe kitu ili usiwe mjinga tena na usimlaumu bashe na serikali yake fahamu haya 1. zambia wana mkataba na kenya wa kulima na kuziana mahindi na soya , hivyo kwa hofu ya mahindi kuadimika kwao n kumbuka wanazalisha kidogo kulinganisha na sisi hivyo wanAzuia kutoka huko kuja bongo ili kumnufaisha mkenya 2. zambia kun uhaba sana wa chakula kwa miaka miwili na bahati mbaya serikali ya zambia haipo sawa kiuchumi kwa sababu ya madeni mAkubwa waliyonayo so hawana akiba ya kutosha kwenye maghara ya serikali hivyo wanahofu mahindi yakiwa expoerted to tanzania na nchi nyingine rwanda , congo na kenya watakuwa na akiba ndogo sana ya chakula kwa kuhofia hilo wana ban mahindi , tanzania hatuna shida ya uhaba kwenye maghara ya serikali so acha wakulima wauze mahindi popote na sisi tutayanunua popote n kupeleka popote
 
Hayo magari yanayozunguka mashambani je
Wakulima wengi huwa hawana mitaji ya kilimo, hivyo wenye pesa huwadhamini kwa makubaliano ya kupeana magunia kadhaa kwa bei kadhaa.

Kwamfano nampa 1000,000 kisha tunakubaliana 50K per gunia kwa mikataba kupitia viongozi wa vijiji, kwahiyo siku akivuna ananipa kwanza zile gunia zangu ndio auze zainazobaki, na mara nyingi unakuta bei iliyopo sokoni ni kubwa kuliko ile aliyofunga nayo mkataba.

Huko Buchosa kwa sasa wanavuna mpunga na bei ya sokoni ni 80K ila kuna jamaa yangu (mfanya biashara ya nafaka) alikwisha kufunga mikataba ya shambani na baadhi ya wakulima kwa kuwapa fedha kwa ahadi ya kumuuza 45K gunia watakapovuna(ili kurudisha ule mkopo).

Huku kwenye field mambo ni tofauti sana na jinsi mnavyoyapamba kwenye makaratasi na nyuma ya keyboard, hapa Tz wakulima wenye misuli ya kuendana na hicho mnachokisema ni wachache mno, wengi wanalia.
 
Magari ya Kenya yamezagaa mashmabni wakinunu nimeona madalali wakilalamika Sana kwa kuwasas HV mkenya anaingia shmbani mwenyewe bila dalali
 
Suala fikirishi sana hapa ni ile wafanyabiashara wa Kenya kufika hadi vijijini mwetu physically kununua mazao toka kwa wakulima. Hii ni dalili kwamba mazingira ya biashara ya mazao ni magumu sana kwa Watanzania lakini rahisi kwa hao Wakenya.

Sidhani kama inawezekana kwa mfanyabiashara wa Tanzania kwenda kununua mazao vijijini Kenya. Tena mazao Wakenya wanayonunua Tanzania mengi ni kwa ajili ya kuuza nje ( re-export).

Serikali ijitafakari. Ideally, wafanyabiashara wa Kenya wangekuwa wakiishia kwenye masoko makuu (wholesale) ya mazao ambapo wangekutana na wafanyabiashara wakubwa wa mazao wa Tanzania na kukamilisha miamala yao huko. Sio masemi trela ya Kenya kuzurura vijijini mwetu kukusanya mazao. Hiyo ingekuwa fursa ya Watanzania.
 
Magari ya Kenya yamezagaa mashmabni wakinunu nimeona madalali wakilalamika Sana kwa kuwasas HV mkenya anaingia shmbani mwenyewe bila dalali
Waache kulalamika kwann na wao wasiende Kenya kusaka soko,madalali wa Kenya wamewazidi nguvu,wawe wabunifu waache kutegemea ndumba.
Huwezi izuia Dunia kuzunguka kisa wewe uzunguki
 


Watz sijui tumelaanika na kitu gani??-- hatujitambui katika mambo rahisi sana. Viongozi wanajua siasa na kukimbiza Mwenge tu.
 
Kama nchi ya Zambia itapiga ban ya kutoruhusu mahindi kuja Nakonde ujue impact yake itakuwa kubwa sana sio tu Kenya ila hata Tanzania .Maana mahindi mengi ambayo wengi tunafikiri yanalimwa Tanzania si kweli ila ni kwmba mahindi yakifika Nakonde yanapita kwa njia za panya yanakuja tunduma ndio yanasafirishwa mikoa mingine na nchi nyingine kwa hiyo demand mwaka huu ni kubwa kuliko supply
 
Kweli itafutwe namna ya kumfanya mkulima anufaike na ukulima wake lakini sio kumkandamiza. !
 
Siku zote mkulima huwa akienda mjini wanam
Shida nini si Ina motivated

Wanafanyiwa hujuma tu wao ndio wanaotoka jasho.
Pana mijitu inanufaika kwa jasho lao tu
huko mjini mkulima huwa anaitwa ni mshamba tu ! Hilo ndilo tatizo kuu !
 

Bei za wakenya na bei za Ndani ya nchi kwa miaka hii ziko sawa tu wala hazina tofauti hivo wazuiwe kutoa nafaka nje hali ya chakula sio hali
 
Huu ujinga unafanywa na wajinga kama Bashe asiekua na akili
 
Niangaike na palizi, mbolea alafu aje mtu aseme nisiuze nje ya nchi huyo mtu atakuwa hazimtoshi
 
Bei za wakenya na bei za Ndani ya nchi kwa miaka hii ziko sawa tu wala hazina tofauti hivo wazuiwe kutoa nafaka nje hali ya chakula sio hali
Kumbuka Kenya Wana export nje matunda na mboga toka kwetu.
Wao connection ya nje kitambo sana kabla yetu
 
  • Je kuna masoko ya kueleweka yanayouza nafaka za jumla? Natamani kuyajua na idadi ya tani zinazouzwa kila siku.
  • Mambo za Ujamaa zilidumazaga akili ya mtanzania mingi.
 
  • Je wakanunue wapi ili hali hakuna wafanyabiashara wala soko (eneo) la nafaka linaloeleweka.
  • Tanzania ina cha kilimo cha kujikimu; ukihitaji, mfano tani 1, 000,000 za mahindi kwa haraka, itakubidi ukazuzure kijijini. Ukiamua kusubiri kwenye hayo wanayoita masoko huyopata na mtaji utakata.
 
  • Je kuna masoko ya kueleweka yanayouza nafaka za jumla? Natamani kuyajua na idadi ya tani zinazouzwa kila siku.
  • Mambo za Ujamaa zilidumazaga akili ya mtanzania mingi.
Ujamaa? Unaingiaje hapa? Nimezungumzia uwezo wa wafanya biashara binafsi wa mazao Tanzania kukusanya mazao toka kwa wakulima kisha kuuza nje. Ndio ujamaa huo? Tofautisha na uamuzi wa kuruhusu wakulima kuuza mazao yao nje which is ok.

Hivi sasa wafanya biashara wa Kenya wanafika hadi vijijini Tanzania na kukusanya mazao kwenda kuuza kwao pamoja na nje (re-export) kama vile ni produce ya Kenya. Hiyo ni failure ya kimkakati upande wetu. Hakuna mfanyabiashara wa Tanzania anaweza kupewa fursa ya aina hiyo Kenya.
 
  • Ikiwa unahitaji tani za kueleweka za mazao, je utazifuata kwenye soko lipi la jumla?
  • Watu wazima wanajua jinsi Ujamaa ukivyoathiri fikra za biashara na uzalishaji. Je una miaka mingapi ndugu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…