Zambia: Rais Hichilema aagiza magari ya kifahari yauzwe ili kulinda uchumi wa nchi

Hakika huyo kaka yetu Hichilema ana kitu tumpe muda.

Rais wa Zambia amewaagiza makatibu wake na mawaziri kuuza magari yote ya kifahari nchini humo.

Magari hayo yaliyonunuliwa na utawala uliopita amesema lazima yauzwe maana ni ya starehe na siyo kuwatumikia wananchi.

Hakika huyo ana kitu angalau cha kumuongelea kwa mema.

 
Huyo ndiyo kiongozi anayetakiwa sasa.siyo huku tanzania rais,waziri,wakurugenzi na wakuu wa mkoa wote wanatembelea magari ya millioni 600 wakati huohuo watoto wanaenda kusoma shule ipo km30-50,hospitali hamna,maji kwa wananchi hakuna na kila kitu kiko vibaya.Bora kuhamia zambia kuliko kukaa nchi ya changamoto lukuki
 
Rais Hichelema ameagiza magari yote ya kifahari nchi humo yauzwe ili kulinda uchumi na kuwataka viongozi waishi maisha ya kawaida kama binadamu wengine huku wakikabiliana na hali ngumu ya uchumi.
Aje wa aina ya Hichilema Tanzania 2025.
 
Kuna faida gani baada ya hapo.

Matajiri wenyewe kwa nchi zetu ndio hao hao wanasiasa au marafiki zao wenye uwezo kununua na kupelekea kuwa mali zao binafsi kwa bei ya kutupa.

Kwa sababu umeuza kwa bei che ata ukinunua mapya cheap hakuna tofauti kubwa.

Gharama zingine zipo pale mafuta, dereva na posho za safari.

Sasa ndio amefanya nini zaidi ya kuruhusu ufisadi tu wa watu kujimilikishia mali za serikali zenye gharama kwa bei nafuu.

Ingekuwa na maana angesema kwenda mbele serikali aito agiza tena magari ya kifahari, lakini kuuza yaliyopo yakiwa bado mazuri huko ni kuchezea hela za walipa kodi tu.
 
Kuuza yaliyopo, Nia ni kununua ya Bei himilivu na low fuel consumption vehicles.
 
Uyu angekuwa Mwenyekiti wa The Green Mamba,tayari mipango ya kumpa Polonium-210 ingekuwa inaandaliwa ili apotezwe!
 
Kuuza yaliyopo, Nia ni kununua ya Bei himilivu na low fuel consumption vehicles.
Provided replacement ni 4x4 sioni savings kubwa ya mafuta ikipatikana. Isitoshe hizi nchi zetu hazina utaratibu wa kupeleka receipt za expenses ofisini kwa ivyo sioni hiyo savings inapatikana vipi.

Muhimu zaidi imagine Tanzania ifanye ivyo, hayo Magari ya tsh 600 hakina nani wanauwezo wa kuyanunua asilimia kubwa ni wanasiasa hao hao, sana sana watajiuzia kwa bei nafuu tu. Huko sasa ndio kujiokotea dodo kirahisi tu na kwenyewe watafanya hivyo hivyo.

Busara ni kutoagiza tena magari ya thamani huko mbeleni, lakini kuuza ni ufisadi tu.
 
Hajanunua magari alikuta faili mezani likisema inabidi kununuliwa magari mapya yazamani yaliyonunuliwa enzi za mtangulizi wake ,akawagomea naona Sasa kaja na kuyauza yote ,zitumike hilux
Huyo ndio Head of State wa mfano katika developing Countries !! Usafiri ni usafiri tu bora ufike unakokwenda hata Hilux ni usafiri tu !! Karma is just around the corner !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…