Da Vinci XV
JF-Expert Member
- Dec 7, 2019
- 3,862
- 6,438
Haikuwa tu Amerika na Umoja wa Kisovyeti katika mbio za kuufika Mwezi na Anga za mbali katika miaka ya 1960.
Kifungu cha habari katika jarida la Time 1964 kilichoelezea kuhusu uhuru wa Zambia kilijumuisha habari nyingine kuhusu mtu mmoja ambaye hakufurahi sana juu ya sherehe hizo za uhuru kwa sababu zilikuwa zinazuia mpango wake wa safari ya anga
Edward Makuka Nkoloso
Huyu mwanadamu alikuwa Edward Makuka Nkoloso, mwalimu wa sayansi na mkurugenzi wa kujitegemea wa Chuo cha Taifa cha Sayansi Zambia, na utafiti wa space na falsafa.
Waandishi wa habari wengi wa kigeni waliichukua habari hiyo na kuandika, ingawa tangu mwanzoni haikuwa wazi jinsi gani ingefanyika na lengo kubwa la Nkoloso lilikuwa lipi hasa ?na ni kiasi gani alikuwa anachezea hadi maslahi ya kimataifa.
Iliripotiwa lengo la Nkoloso lilikuwa kufanya Zambia iwe nchi ya kwanza kufikia mwezi. Labda baada ya uhuru Nkoloso alikuwa na nia ya kuthibitisha nguvu na umuhimu wa nchi katika hatua ya dunia.
Katika jaribio la kufikisha ujumbe huu kuwa anaweza kuufikia mwezi Nkoloso aliajiri astronauts(wanaanga) kumi na mbili, na kuanza kuwapa mafunzo aliyoyapanga yeye mwenyewe
Aliwaweka katika ngoma yenye mafuta, akawaweka kwenye miti iliyochimbwa kati miti na kuibiringita mpaka chini ya milima ili kuwaandaa kwenye swala la uziito na mafunzo mengi mengi.
(unaweza kutembelea youtube kujionea)
MATHA MWIMBA MWANAANGA ALIYEISHIA KUPATA MIMBA
Matha Mwimba mwenye umri wa miaka 16 alichaguliwa kama mtu wa kwanza kujaribu kwenda Mars. Nkoloso alidai kuwa mwishoni mwa mwaka wa 1964 msichana huyo pamoja na paka wawili na mjumbe wa Kikristo, wangefanya safari ya kwenda mwezini na kisha kwenye Sayari ya Mars. Mbwa wa Nkoloso aliyeitwa Cyclops wakati huo alifanya Spacecraft iliyotaka kutumiwa na Nkoloso kupewa jina mbwa huyo - Cyclops I
NKoloso aliripotiwa kuandika kwa nchi nyingi na mashirika ya kuomba pesa,
Aliwaandikia Israeli , Marekani, USSR na UNESCO. kuhusu kupata Mchango aliomba ombi la kupata $ 20,000,000 hadi dola bilioni 2
, Yeye hakupokea chochote lakini alikuwa anahitaji sana. Licha ya kuomba fedha kutoka kwao, Nkoloso alitoa tuhuma juu ya Marekani na Soviet Union, akisema aliamini kwamba walitaka kuiba siri zake na kuufikia uso wa mwezi wa kwanza kabla yake. Mpango huo hatimaye ulifeli na si tu kwa sababu ya ukosefu wa fedha. Hata mwanaanga aliyechaliwa Matha Mwamba akapata mimba na kurudi nyumbani kwao
Wanaanga wengine pia waliondoka, waliripotiwa kuendelea na maisha mengine kamwe hawakurudi, Na hapakuwa na wavumbuzi na wala hakuna pesa, mwezi ukaonekana upo mbali sana.
Baada ya kushindwa kwa mpango wake safari ya Anga, Nkoloso alihamia katika siasa - alichaguliwa kwa kituo kimoja cha ukombozi, ambacho kilizingatia uhuru wa kikanda.
Afronauts Nkoloso baada ya majaribio ya kusafiri SPACE kushindwa akataka iwe sehemu ya historia iwe yenye kusahauliwa tu, na haikuwa kawaida katika makala ya zamani
Lakini waasanii kama vile Cristina de Middel. wakatoa Mfululizo wa hadithi za picha 2012 na Middel aliuita 'Afronauts' - jina lile lile Nkoloso alilowapa astronauts wake - ikaibuka hadithi hii tena. Baada ya kuja na mpango wa Anga wa Zambia katika orodha ya majaribio yaliyoshindwa, De Diddel alihisi kulazimika kutengeneza hadithi.
Picha ya 'Afronauts' ilikuwa imechapishwa na De Middel na alipata sifa nyingi.
da Vinci XV