MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Pichani ni wananchi kwenye miji mbalimbali nchini Zambia wakiwa kwenye foleni za kununua unga wa mahindi. Kwa sasa Zambia inakabiliana na uhaba mkubwa wa unga wa mahindi maarufu kwa jina la MEALIE MEAL.
Inadaiwa kuwa uhaba huo umetokana na Serikali kuruhusu uuzwaji holela nje ya nchi wa mahindi toka kwenye akiba ya taifa. Sababu nyingine imetokana na uhaba wa mahindi kwa nchi ya Tanzania kutokana na Tanzania & Zambia kuwa nchi mbili pekee kwa ukanda huu zinazolima mahindi halisi na sio GMO.
Kwa sasa taifa hilo limezuia uuzwaji wa mahindi au unga wa mahindi nje ya nchi hasa katika nchi ya DRC. Ikumbukwe DRC ni mnunuzi mkubwa wa miaka yote wa mahindi toka Zambia. Mpakani mwa DRC & Zambia katika mji wa Kasumbalesa kuna kamata kamata kubwa kwa malori yanayotaka kuvusha mahindi na unga kihuni kuelekea DRC. Pia watu binafsi wenye shehena za unga wamekuwa wakikamatwa na kupewa tuhuma za ulanguzi kitu ambacho kimepingwa na wengi na kuonekana ni uonevu.
Tanzania tunaishukuru Serikali ya Chama Cha Mapinduzi kwa uongozi imara na kuivusha nchi kwenye aibu ndogondogo kama hizi. Kwa sasa Zambia inaongozwa na HH wa chama cha UPND ambacho kinasifiwa sana na wapinzani wa CCM hapa nchini bila kujua wanachosifia.