PreGE2025 ZAMECO yatoa wito wa Sheria rafiki ya habari Zanzibar katika kipindi cha uchaguzi

PreGE2025 ZAMECO yatoa wito wa Sheria rafiki ya habari Zanzibar katika kipindi cha uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Habari Hub

Member
Joined
Oct 28, 2015
Posts
11
Reaction score
0
Na Mwandishi wa Habari Hub

Kamati ya Wataalamu wa Masuala ya Habari Zanzibar (ZAMECO) imeungana na jamii ya kimataifa kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani Mei 3, 2025, kwa kutoa wito wa kuwepo kwa sheria rafiki ya habari itakayochochea uchaguzi huru na wa haki Zanzibar. Kwa kaulimbiu inayosema “Sheria nzuri ya Habari ni chachu ya uchaguzi ulio huru na wa haki”, ZAMECO inalenga kuchochea majadiliano ya kitaifa kuhusu mazingira salama ya habari kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba.


Katika taarifa yao, ZAMECO imesisitiza haja ya kuwa na Sheria Mpya ya Habari Zanzibar inayozingatia Katiba, mikataba ya kikanda na kimataifa, pamoja na maoni ya wadau waliotoa mchango wao katika mchakato wa muswada. “Sheria hiyo itasaidia kujenga msingi wa uchaguzi ulio huru, wenye haki na uwazi,” imesema taarifa hiyo ya Mei 3, 2025.


Kamati hiyo pia imetoa wito kwa vyombo vya dola na vyama vya siasa kuhakikisha waandishi wa habari wanalindwa dhidi ya vitisho, mashambulizi au unyanyasaji katika kipindi cha uchaguzi na baada yake. “Waandishi wa habari ni nguzo muhimu ya demokrasia. Wana haki ya kufanya kazi zao bila hofu,” imeeleza taarifa hiyo.


ZAMECO imekemea pia ubaguzi kwa waandishi wa habari kwa misingi ya itikadi au aina ya chombo cha habari, ikitaka kila mwandishi mwenye sifa kupewa kitambulisho cha kuripoti uchaguzi. “Tunatoa wito kwa Tume ya Uchaguzi, vyombo vya dola na watoa taarifa kuwa wawazi na kutoa ushirikiano kwa vyombo vyote vya habari bila upendeleo,” imesisitiza.
 
Back
Top Bottom