Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Lengo kuu la mradi huu ni kuhakikisha tunajenga kizazi chenye ufahamu wa kutosha kuhusu masuala ya afya ya akili, tunapunguza unyanyapaa, na tunawawezesha vijana pamoja na walimu kutambua umuhimu wa utunzaji wa afya ya akili katika mazingira ya shule.
Tunashukuru kwa ushirikiano wa Wizara ya Elimu na Wizara ya Afya, pamoja na wadau mbalimbali ambao wamekuwa sehemu ya safari hii. Pia, tunatoa shukrani za dhati kwa shule zinazoshiriki katika mradi huu kwa kujitolea kushirikiana nasi katika kufanikisha lengo hili muhimu.
Tuna imani kuwa mradi huu utaacha athari chanya na kuleta mabadiliko ya kudumu katika shule na jamii kwa ujumla. Tunaendelea kuwakaribisha wadau mbalimbali kuungana nasi kwa namna yoyote ile kuhakikisha tunapanua wigo wa mradi huu kwa manufaa ya kizazi kijacho.
Asanteni sana, na tutaendelea kushirikiana nanyi ili kuhakikisha tunafanikisha malengo yetu!
Mkurugenzi Mkuu wa ZAMHSO, Mwalimu wa Saikolojia wa Chuo Kikuu cha Abdurahman Al-Sumait, na Mwanasaikolojia kutoka Hospitali ya Ampola Tasakhtaa, Zaituni Shabani Salum amesema:
“Watoto wengi huja shuleni wakiwa wamebeba “mabegi yasiyoonekana” yaliyojaa changamoto. Msongo wa mawazo, wasiwasi, hofu, wasiwasi mwingi, majeraha ya kihisia, mahitaji ya msingi ambayo hayajatimizwa, upweke, hasira, huzuni, na kukata tamaa huwafanya kuwa na uzito mkubwa; uzito ambao huzuia kujifunza kwa ufanisi.
Watoto hawa wanahitaji ushauri nasaha pamoja na msaada wa kisaikolojia
Waangalie, watambue changamoto zao, na uwapende badala yake.”
Pia soma:
~ Zanzibar Mental Health Support Organization imeanza kutekeleza Rasmi Mradi wa Elimu ya Afya ya Akili Shuleni
~ Zaituni Shabani Salum wa ZAMHSO: Elimu ya Afya ya Akili ni nguzo muhimu kwa kizazi chetu