ZANTEL wamepunguza bundle la Wiki kutoka GB 2.2 kwa Tsh 3,000 hadi GB 1.9 kwa Tsh 3,000

AFYA ZAIDI CONSULTANTS

Senior Member
Joined
Mar 6, 2017
Posts
138
Reaction score
527
Daahhh sisi tunaotegemea kujifunza, kufanya marketing na sales kwa njia ya mtandao gharama zimepanda tena. Leo naamka nakuta kifurushi cha Wiki cha ZANTEL ambacho ilikuwa unapewa GB 2.2 kwa Tsh 3,000 (Hapo kilipunguzwa pia kutoka GB 2.5) kwa sasa unapewa GB 1.9 tu. Sasa na haya mambo ya YouTube, Instagram na Streaming GB 1.9 ni kifurushi cha siku 3 tu.

Halafu haya makampuni ya simu ni wajanja kweli. Wao hawaongezi bei, bali wanapunguza ukubwa wa bundle/idadi ya GB. Maana wanajua wakiongeza bei mauzo yao yatapungua zaidi.

Huko VODACOM, HALOTEL, AIRTEL na TTCL Vipi?
 
Nafikiri ni mitandao yote imepunguza GB, na bei imebaki ile ile huwa wanaambiana kabisa🤣
 
2GB = TZS. 2,640 ( buffee )
Ila ujinga wao huwezi kuangalia Salio hadi upige customer care uongee na mhudumu akwambie Salio la bando, sms, muda wa maongezi na T-pesa maana menu yao ipo off mwezi sasa(sijuhi no makusudi au wamenunuliwa kuliua shirika!)
 
Daahhh sisi tunaotegemea kujifunza, kufanya marketing na sales kwa njia ya mtandao gharama zimepanda tena. Leo naamka nakuta kifurushi cha Wiki cha ZANTEL ambacho ilikuwa unapewa GB 2.2 kwa Tsh 3,000 (Hapo kilipunguzwa pia kutoka GB 2.5) kwa sasa unapewa GB 1.9 tu. Sasa na haya mambo ya YouTube, Instagram na Streaming GB 1.9 ni kifurushi cha siku 3 tu.

Halafu haya makampuni ya simu ni wajanja kweli. Wao hawaongezi bei, bali wanapunguza ukubwa wa bundle/idadi ya GB. Maana wanajua wakiongeza bei mauzo yao yatapungua zaidi.

Huko VODACOM, HALOTEL, AIRTEL na TTCL Vipi?
sio Zantel tu hata Vodacom
 
Ila ujinga wao huwezi kuangalia Salio hadi upige customer care uongee na mhudumu akwambie Salio la bando, sms, muda wa maongezi na T-pesa maana menu yao ipo off mwezi sasa(sijuhi no makusudi au wamenunuliwa kuliua shirika!)
Hata menu za bank huwezi kuingia.
 
Ila ujinga wao huwezi kuangalia Salio hadi upige customer care uongee na mhudumu akwambie Salio la bando, sms, muda wa maongezi na T-pesa maana menu yao ipo off mwezi sasa(sijuhi no makusudi au wamenunuliwa kuliua shirika!)
Mbona kwangu naona salio vizuri tu, naangalia salio la kawaida kwa kubonyeza *102# then wananitumia meseji ya salio la bando.

Now niko Znz toka jana naona hakuna network, ningekuwa bara ninge screenshot uone.
 
Salio linakuja ndio hamna shida labda kwa badhi tu ndio inazingua
 
Ila ujinga wao huwezi kuangalia Salio hadi upige customer care uongee na mhudumu akwambie Salio la bando, sms, muda wa maongezi na T-pesa maana menu yao ipo off mwezi sasa(sijuhi no makusudi au wamenunuliwa kuliua shirika!)

Mkuu unaangalia kwa kupiga *102# tu kama kuangalia salio la kawaida unatumiwa meseji yenye maelezo kamili mimi pia mwanzo nilizani ivyo ila kumbe ukiuliza salio kama salio kuu unaletewa kila kitu jaribu
 
Oya wameambizana kote mpk Tigo nao wamepandisha gharama.
 
Mkuu unaangalia kwa kupiga *102# tu kama kuangalia salio la kawaida unatumiwa meseji yenye maelezo kamili mimi pia mwanzo nilizani ivyo ila kumbe ukiuliza salio kama salio kuu unaletewa kila kitu jaribu
Nimefanikiwa mkuu, naona huduma imerejea, hahaha!
 
Back
Top Bottom