Naomba niulize swali la msingi hapa, naona kuna kitu sikielewi vizuri.
Nnavyofaham, nikiwa na line ya voda, tigo, airtel au mtandao wowote, nikituma au kupokea pesa nikiwa mahali popote, makato ni yale yale kwakuwa imewekwa hivyo kwenye system.
Kwa mjadala unavyoenda ni kama watu wa Zanzibar wakitumiana pesa hukohuko hawakatwi tozo la uzalendo, hii inawezekanaje?
Nikiambiwa mtandao wa Zantel haujafanya hayo mabadiliko, hiyo naweza kukubali lakini mitandao mingine haijalishi uko eneo gani la nchi, tozo iko pale pale.