Zanzibar: Askari wanne wa SMZ na maofisa 3 wa Idara ya Misitu mbaroni kwa mauaji ya Katibu wa ACT-Wazalendo tawi la Mwembemakumbu

Amebainisha kuwa askari hao walichukua mkokoteni huo kwa lengo la kuupeleka katika ofisi zao zilizopo Maruhubi lakini muda mfupi baadaye walivamiwa na kundi la vijana wakiwa na mapanga na silaha mbalimbali, akidai kuwa walitaka kuwazuia polisi na maofisa hao kutoondoka na gari walilokuwa wamepanda.

Kwa hii kauli tayari polisi washamaliza mchezo.
 
Waninga hawa, wanatafuta Kiki tu.
 
Habari njema,..

Vile vile wawajibishe na wale wotewalio uwa na kuwatesa raia wasiokuwa na hatia wakati wa Uchaguzi..

Nchi inaendeshwa na Sheria ndio inaoongoza Nchi
Ndio maana Sheria ukisema usiandamane, ukaenda, kinacho kupata ni halali yako
 
Imekuchoomaaa kama pasi eeeeh?? Meza tikiti maji basi...
 
ALAFU SIJUI KWA NINI ASKARI HASA POLISI HUWA HAWASTUKI ....YAANI KAZI YAO IKISHAKUWA IMEISHA WANAWATOA KAFARA KAMA USHAHIDI .....KAMA YULE POLISI ALIYEMUUWA MWANDISHI WA HABARI IRINGA.....KAMA KWELI WAKO SERIOUS WAKAMATE MAZOMBI WOTE ....
 
Maelezo dhaifu sana, hivi kweli vijana wenye mapanga na marungu wanaweza kujitokeza hivyo kwa suala la mkokoteni wenye mchanga!
 
Tayari hapo Polisi wamekwishadai eti wao ndo walishambuliwa
 
Picha za watuhumiwa ziko wapi?
Nimemkumbuka Kamanda Muroto
 
Walimjua Ni act WAZALENDO ndo maana wakampiga risasi
 
Maelezo yanasema alikimbia.....
Sasa tunaona tena kapigwa risasi!
 

Jamani hivi ni hadi lini hawa jamaa wanapotowa taarifa zao za uongo wanafikiri kuwa sisi wananchi hatuna uwezo wa kujua kama wasemacho ni uongo?

1. Tunaambiwa kuwa wananchi walijitokeza na mapanga na silaha mbali mbali. Suali video hio hapo mbona hakuna hata mmoja mwenye silaha yeyote hata fimbo?

2. Tunaambiwa kuwa askari hao walichukua mkomkoteni kwa lengo la kuupeleka kituoni kwao. Suali hivi walikuwa wanataka kumpakia punda na mkomkoteni wake katika gari yao?

3. Tunaambiwa kuwa Slemani alikimbia alipowaona askari na aliwacha mkokoteni na punda wake, sasa ajabu ni kuwa tunazidi kuambiwa kuwa baada ya wananchi kuwavamia askari hao walifyatua risasi amabyo ilimpiga Slemani. Suali Hivi askari hawa wana shabaha ya aina gani kiasi cha kuweza kufyatua risasi na ikawakosa wale wote waliowavamia na kumpata Slemani ambae alikwisha kimbia katika eneo hilo?

4. Kama walivyatua risasi baada ya kuvamiwa na wananchi ni kwa nini hivi sasa wako mahabusu? Kwa nini hawakusimamishwa kazi tu wakati uchunguzi unaendelea?

Msitufanye sie watoto wadogo jamani!!!!!

Kwa taarifa tunazozipokea ni kuwa Slemani hata hakupigwa risasi hapo alipokutwa, ila askari walimtupa hapo baada ya kumpiga risasi sehemu nyengine kabisa.
 
Japo taarifa inajikanganya sana kwenye majina na tittle ya muhusika ila kitendo cha kumuuwa binaadam yeyote ni ukosefu wa utu. Nimejaribu kutazama hapo kwa hao watu sijaona hata mmoja mwenye jiwe sembuse mapanga yaliyotajwa. Pia inaonesha aliyeuawa sio aliyekimbia na kama ni aliyekimbia kwa kukutwa na mkokoteni wa mchanga ni wazi aliuwa mapema kabla ya wananchi kuwazingira hao askari.

Kama nchi tumefikia hatua mbaya sana ambayo wenye mamlaka ya kutulinda wanaona rahisi sana kutuuwa. Inaumiza sana.... Poleni sana wafiwa.
 
Hivi wewe ulisoma hiki ulichokiandika hapa kabla ya kubonyeza "post reply"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…