Zanzibar: Barabara iliyopo Kwerekwe Makaburini inakuwa hatarishi kwa kuwa Madereva wengi hawazingatii Zebra

Zanzibar: Barabara iliyopo Kwerekwe Makaburini inakuwa hatarishi kwa kuwa Madereva wengi hawazingatii Zebra

MeVSMe

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2024
Posts
270
Reaction score
425
Huku kwetu mitaa ya Kwerekwe Makaburini kuna mistari ambayo inatumika kuruhusu Watu kuvuka Barabarani maarufu kwa jina la Zebra.

Hapo nazungumzia barabara ya kubwa ya kwenda Fuoni, lakini cha ajabu madereva wengi hawasimamii Sheria za barabarani ikiwemo kutozingatia matumzi ya Zebra hizo zilizopo.

Kutokana na dharau za madereva zimeshatokea ajali nyingi maeneo hayo na wengine wamenusurika kugongwa na magari lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.

Zebra zipo karibu na Kwakipogo ambapo kuna idadi kubwa ya Wanafunzi ambao huwa wanatakiwa kuvuka hapo lakini hawavuki kwa kutumia Zebra bali lazima wapewe msaada wa mtu mwengine ambaye anaingilia kusimamisha magari ndio Wanafunzi wanavuka.

Hili lifanyiwe kazi ikiwezekana kuwe na trafiki ambaye atakuwa anawajibika hapo au kamera zilizopo zitumike kuwawajibisha madereva ambao hawazingatii Sheria.
 
Back
Top Bottom