Zanzibar kuna jambo lawezatokea, mwaka huu.
Kikwete aliturudisha nyuma sana aliposhindwa kuheshimu Uchaguzi wa Zanzibar na kukubali Jecha kufuta ucbaguzi kinyume cha sheria.
CCM wakashinda kwa hila wakati Shein alipaswa kuwa Makamu wa Rais na nchi ikasonga mbele na Wazanzibari wakaendelea kuwa wamoja.
Sasa wananchi wa Zanzibar albao Kiuhalisia wana maisha Magumu sana huku Viongozi wao wanaotokana na Chama cha mapinduzi wakijineemesha na kutumia Jeshi la Polisi kuwatesa wananchi.
Tuliombe Jeshi la Polisi kuacha kutumia Risas kuwabeba CCM.
Siku watakapogundua kuwa CCM ni hatari kwa kila mwanadam hata kwao wenyewe ndipo watakapoona kuwa walichelewa sana kuachana na siasa za uonevu.
Wanaoumizwa na Amani kuvurugika Zanzibar Sio Mabilionea waliojificha Chini ya CCM bali ni polisi wenyewe wanaojiingiza kwenye uhasama na wananchi na kujikuta wakifarakana na kila mtu.
Hivi kweli kuna askari wadogo kwenye jeshi lolote anayetumia akili yake na kutafakari amaweza kuvuruga jamii ili Mtoto wa Rais ,Hasan Mwinyi aliyekaa kwenye Uwaziri kwa miaka 25 na kuishi maisha kama Peponi tangu kuzaliwa ,eti awe Rais kwa dhulma ?
Askari anayeweza kuwaua watu ili tu Mwinyi apate Urais atakua anajipandikizia laana kubwa san a Duniani na Ahera. Hata Mungu atakua anamcheka huyo askari. Hata shetani na uovu wake hajafikia kiwango cha ubaya wa askari wanaowatetea walioshiba na kuwadhulumu wenye njaa .
Polisi tambueni tu kuwa Mwinyi hana alichokosa zaidi tu ya uroho na ubinafsi wa roho za binadam wasio mcha Mwenyezi Mungu kukosa shukrani na kuridhika hata angepewa dunia nzima nado haridhiki.
Polisi wanapozidi kukubali kutumiwa na raia wahalifu waliojificha chini ya CCM wajue kuwa wanawagawa wazanzibari na wanatengeneza Chuki kubwa sana badala ya umoja. WanaCCM kwa uhalifu wao wanatumia madaraka yao kuwaamrisha askari kuwaumiza wananchi ili tu kulinda maslahi yao na madarka yao.
Mfano ni Kule chato WanaCCM na wauaji wakubwa waliotaka kumuua Lisu miaka mitatu iliyoputa waliendeleza uhuni wao lakini hatukusikia kuwa wamekamatwa wala kutafutwa zaidi ya maneno ya kusema amani bila vitendo.