Zanzibar inachangia nini kwenye Serikali ya Muungano? Isije ikawa wanatumia Kodi za Bara

Zanzibar inachangia nini kwenye Serikali ya Muungano? Isije ikawa wanatumia Kodi za Bara

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Watu tunataka Elimu mchango ambao Zanzibar inatoa kwenye Serikali ya Muungano. Naona kama Tunaumia sana sisi wa Bara. Kuubeba Muungano.

Mfano nataka kuoa. Nimeandaa Harusi baadaye nikaamua kutofanya sherehe. Je zile pesa nagawa pia kwa bibi harusi? Ndicho ambacho alichofanya Samia. Yaani pesa hizi ambazo zimeandaliwa na Watanzania Bara kwa Sherehe isiyo na tija kaamua zigawanywe sawa kwa sawa.

Hili suala tuanze likemea mapema. Kodi za Wabara zitumike kwa Wabara. Na Wazanzibar zitumike kwao kwa maendeleo ya nchi yao.

Tabia ya kupendelea eneo moja analotoka Rais ikomeshwe isiendelee.tuliona miradi mingine ilivyokuwa ikipelekwa sehemu ambazo hiyo miradi haikuwa na tija.

Lakini suala langu kubwa ni kupeana Elimu kuwa kuna pesa gani ambazo Bara inapata toka Zanzibar? Au zinaingia kwenye Muungano toka Zanzibar?

But pia hizi pesa anazotaka zipelekwe Zanzibar pia. Zilitokea au patikana wapi? Kodi za Wabara zisitumike vibaya. Watu kwa sasa kwa woga au Unafiki wanashindwa kuhoji hili jambo.

Ila wajue mwanzo wa ngoma ni lelele.... Tusikubali mambo ya hovyo kuendelea. Na mchakato wa Katiba urudishwe ili haya mahusiano yawe yame balance. Zanzibar wasionewe hali kadhalika Bara pia wasionewe. Hawa wabara ndo hata Serikali yao hawana.
 
Mkuu Zanzibar inachangia Jina maana hebu piga picha tu Tungeendelea kuitwa "Tanganyika" jina lenyewe linahuzunisha kabisa
nakuunga mkono huyo jamaa hailewii kwamba hilo jina tuTanzania ni pesa na bara wameamuwa kulitumia miaka nenda miaka rudi na kuachana na tanganyika huyu mama kweli ana wasaidizi wa shoka hongera mama sasa zanzibar itapata haki zake zote inazostahiki.
 
Muungano huu una babaishaji mwingi sana yaan kiufupi wazanzabari ndio wanapata faida sisi wabara tunafaidika labda na jina la Tanzania na kuongezeka kwa eneo la bahari hakuna faida kwa watanganyika maana vitu vingi wazanzibar wanaruhusiwa huku kwetu wakati sisi kule kwao huruhusiwi kama kazi, ardhi au kununua bidhaa.

Unyonyaji mkubwa sana inabidi wakae chini tena waangalie kasoro.
 
Tuliaaaaa tuli mlipoamua kujivisha koti la muungano na kusahau nchi yenu ya Tanganyika mlitegemea nini? hizi ni sherehe za muungano , Zanzibar kama sehemu ya Muungano wanayo haki kupata pesa hizo, kama hutaki tafuteni jina lingine lakini sio lenye neno muungano
 
Muungano huu hauna faida kwa watanganyika. Unawafaidisha wazanzibari tu.

Anayebisha anyooshe mkono juu, au hata afanye kama anajikuna. Halafu alete faida moja tu ambayo mtanganyika anaipata.
Mkuu tumeona miaka hii sukari ni shida na bei ya juu, lakini Znz wana sukari na bei ya chini.

Sheria hairuhusu wa Znz kutuuzia sisi sukari, ila sisi tunaruhusiwa kuwauzia wao.

Je unahisi nani anafaidika? Viwanda vya Znz ama vya huku kwetu?
 
Muungano huu hauna faida kwa watanganyika. Unawafaidisha wazanzibari tu.

Anayebisha anyooshe mkono juu, au hata afanye kama anajikuna. Halafu alete faida moja tu ambayo mtanganyika anaipata.
Zanzibar wanapoomba msaada kutoka nje ya nchi lazima msaada ule upite tanganyika kwanza uvhukuliwe nusu na robo thn znz ndio wanapata kilichobaki, TRA kukusanya mapato ikiwemo sector ya utalii znz

Sent from my SHARK MBU-H0 using JamiiForums mobile app
 
Zanzibar wanapoomba msaada kutoka nje ya nchi lazima msaada ule upite tanganyika kwanza uvhukuliwe nusu na robo thn znz ndio wanapata kilichobaki, TRA kukusanya mapato ikiwemo sector ya utalii znz

Sent from my SHARK MBU-H0 using JamiiForums mobile app
Hizi ndio kero za muungano kama anaomba Zanzibar ilipaswa iende Zanzibar na pia watalii kama walikuwa dhumuni ni kwenda Zanzibar inabidi pesa ya utalii iende zanzibar
 
Muungano huu una babaishaji mwingi sana yaan kiufupi wazanzabari ndio wanapata faida sisi wabara tunafaidika labda na jina la Tanzania na kuongezeka kwa eneo la bahari hakuna faida kwa watanganyika maana vitu vingi wazanzibar wanaruhusiwa huku kwetu wakati sisi kule kwao huruhusiwi kama kazi,ardhi au kununua bidhaa
Unyonyaji mkubwa sana inabidi wakae chini tena waangalie kasoro
alaf cha ajabu sasa kila wakikaa kikao kuhusu changamoto za muungano wanajadil zile ambazo zinaonekana tatzo kwa Zanzibar inaonyesha upande wa bara kama vile wanalazimisha muungano labda kwa kuna sababu ambazo sisi wananch hatujui,na kusema et jina ndio mojawapo ya faida haina faida sana kwa sababu bila neno tanganyika kuwepo ata ile neno tanzania lisingekuwepo so labda tusingeungana lingebak tanganyika au lingetoa jina lingne na jina halina athari kiuchum au kimaendeleo
 
huyu mama nchi itamshinda mapema kama ataendelea na huu ujinga aloanza nao
Kwani kafanya nn, kila anachokifanya mama kimo kikatiba, sio kama yule mzee anafanya ubabe wake, ndio mjue kuwa katiba au makubaliano ilikua hayafuatwi, sasa vile walivyokubaliana ndio wanajaribu kufata now

Sent from my SHARK MBU-H0 using JamiiForums mobile app
 
Mnalalamika Zanzibar haina mchango wowote kwenye Muungano,ila AJABU NI KWAMBA WAZANZIBARI WAKITAKA KUJIONDOA KWENYR HUO MUUNGANO MNATUMIA HADI MITUTU KUHAKIKISHA HAWAONDOKI.

CCM na viongozi wa serikali wanaotoka Bara akili zao si timamu!
Iyo sio kwa zanzabar tu ni ngumu sana ktu kikiwa pamoja au kikiungana kutaka kujitenga si kaz ndogo ,mfano angalia tigray au catalunya na kwingneko
 
Zanzibar wanapoomba msaada kutoka nje ya nchi lazima msaada ule upite tanganyika kwanza uvhukuliwe nusu na robo thn znz ndio wanapata kilichobaki, TRA kukusanya mapato ikiwemo sector ya utalii znz

Sent from my SHARK MBU-H0 using JamiiForums mobile app

Kumbuka sisi ni Tanganyika wala si Tanzania. Katika Tanzania, na Zanzibar wamo.

Sasa kama msaada waja kwanza Tanzania halafu tena sehemu yaenda Zanzibar, huoni kuwa Zanzibar wao wanapata mara mbili hali sisi hamna kabisa.

Kinachokwenda Tanganyika kipo wapi?

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Hakuna haja ya kulaum hata kama wangepewa wasichochangia sababu ni sisi wenyewe wa Bara ndio tuna matatizo! Mzeae Warioba alituletea katiba ya serikali tatu ambayo kimsingi ingeweka wazi mipaka na majukumu ya serikali zote tatu, serikali ya bara, ya Zanzibar na ile ya Muungano sasa sisi tukabisha na kuleta mizengwe mpaka mchakato ukavurugika, acha tuvune tulichopanda!
 
Back
Top Bottom