Zanzibar inastahili 50% ya Muungano

Mimi naaamini Nyerere alikosea sana kuwaunganisha wazenji na watanganyika kaipa Tanganyika mzigo mzito.hii nchi ingejitenga wafanye yao kwa maendeleo ya watu wao
Ajabu Zanzibar haina mwenyewe hao wote wanaopiga kelele ni wahamiaji, wengine walihamia kama watumwa,wengine kama washihiri na wengine kama wavuvi, narudia tena wote ni wahamiaji pale Zanzibar kuna watu wana asili ya Malawi, Tanganyika, Congo, Comoro,China,Oman,India etc. Ila kwa sasa mazingira yamebadirika ilitakiwa waachiwe kijiji chao.
 
Na kule Zanziberi mteue 50/50 watanganyika tuwemo serikali ya mapinduzi
Ohoo! Hapa ndipo mnapojifanya hamuelewi na tulishawapa solution zamani tu. Serikali ya Zanzibar ni serikali ya wananchi wa zanzibar,nyinyi si wazanzibari. Serikali ya Tanzania ni wa wananchi wa Tanzania, sisi na nyinyi ni watanzania. Tumekuambieni zamani tu kuweni na serikali ya Tanganyika kwa ajili ya wananchi wa tanganyika, lakini hamtaki,, sasa unataka upewe madaraka katika serikali isiyokuhusu kwa sababu gani hasa?
 
Mbona sijawahi ona mtanganyika kateuliwa Zanzibar? Mtanganyika hata ardhi Zanzibar hapati! Hiyo 50 50 ya wapi? Kunjueni nyanyueni jamvi kwa amani

Mkuu Hivi hujui kama MZee Mwinyi na Mwinyi Jr ni Watanganyika ?
 

Tanganyika mwenyewe nani?
 
Waziri wa Muungano tu labda ,unafaa, Ila mengine kila mtu ajitegemee
 
Ningelikushauri kwanza usome historia kabla ya kuropokwa hapa. Muungano wa zanzibar na wadanganyika ulifanyika baada ya sisi kumpindua sultani. Ukumbuke kuwa nyinyi mmepewa uhuru wenu kwa karatasi. Siku karatasi yenu ikiliwa na mchwa msishangae mzungu kurudi kukutawalieni tena. Sisi tumepata uhuru wetu kwa kupindua serikali!

Kuhusu kujitenga kwa nini kwanza huwaulizi viongozi wenu ni kwa nini hawataki tujitenge? Toka enzi za nyerere tumelianza hilo na mpaka leo mnakataa? Kama kweli tunawarudisha nyuma na ni mzigo kwenu kwa nini viongozi wenu bado wangangania muungano huu? Kwa nini viongozii wenu walikataa kuonyesha mkataba wa makubaliano ya muungano yaliotiwa sahihi na nyerere pamoja na karume?

Usije kunipa jawabu eti sisi ndugu, sisi tuna udugu wa kweli wa wakenya kuliko nyinyi watanganyika.

Hivi wewe kama una mke ambae hana afanyalo la kukusaidia katika maisha ye nu zaidi ya hasara na madeni kila siku, na kila kukicha anadai talaka yake, hivi kweli utabaki nae au utamfungia mabegi na kumfukuza kwako? Sasa kama kweli sisi tunawaletea hasara na kukurudisheni nyuma, kwa nini mnangangania kubaki nasi?
 
I hope wadanganyika wote hawana akili kama zako, na angalau wanajua historia yao. Hivi tanganyika ni ya akina nani? Hebu nenda kasome historia ya afrika na tanganyika kwanza nautajua wapi babu wa mababu zako walikotokea na vipi walifika sehemu hizi za afrika ya mashariki.
 

Naona umesahau na madeni ya nchi, vipi pia tugawane 50-50. Tukidai 50/50 basi na tudai 50/50 ya kweli.
 
Kwenye Muungano mnacontribute nini.

Nyie leteni fyokofyoko.

Tutaifanya unguja na Pemba mikoa na nyodo zenu zitai siri kuwa zimeisha
Ikiwa hatuleti kitu kwa nini mnangangania muungano, kwa nini hamkubali kuuvunja muungano? Sema tu ni nini Tanganyika mnachokipa kisirisiri katika muungano huu?
 
Yah right........ Na kwenye bajeti wachangie 50 % pia .....!!
 
Hilo haliwezekani kamwe. Msimharibie SSH
 
Ikiwa hatuleti kitu kwa nini mnangangania muungano, kwa nini hamkubali kuuvunja muungano? Sema tu ni nini Tanganyika mnachokipa kisirisiri katika muungano huu?
Kwa sasa hakuna,ila wakati ule tulipoungana tuliwafanya kama ngao ya mashambulizi toka bahari si unajua Tanganyika ilikuwa makao makuu ya ukombozi wa Afrika.
 
ok ok hebu natuangalie kwa upande huu

biashara sio jambo la muungano lakini stone town yote mumeiteka na kufungua vijiduka feki kuuza vinyago na picha za michoro ya ovyo kwa watalii. Kadhalika mmeanzisha madanguro na uuzaji wa madawa ya kulevya mnayoyaficha kwa pretence ya maduka ya utalii.

Elimu si jambo la muungano lakini watoto wenu mlokuja nao wamejaa katika shule zetu za serikali.

Ujambazi si jambo la muungano lakin kila siku mnakua kwa meli kutuibia na kuua ndugu zetu kisha mnakimbilia kwenu bara.

ardhi si jambo la muungano, lakini kila kukicha mnakuja na kujenga ovyo ovyo vijumba katika sehmu ambazo hazikupimwa au kupewa wananchi (wazanzibari) kihalali.
 
Kwa sasa hakuna,ila wakati ule tulipoungana tuliwafanya kama ngao ya mashambulizi toka bahari si unajua Tanganyika ilikuwa makao makuu ya ukombozi wa Afrika.
Good point na kweli ilikuwa inafahamika sana wakati ule wa east and west block, tanganyika ilihitaji zanzibar ili kujiliannda na mashambuli ya baharini. Lakini kwa sasa kwa nini bado watu wangano?angania huu muung
 
Kwani hao wazenji wanamchango gani kwenye muungano?tunahitaji kujua then tujue tunafanyeje kwenye hilo swala la pasu kwa pasu.nawasilisha
 
🤣🤣🤣
Mkuu Zanzibar ni sehemu ya Tanzania ....

Wazanzibari kama walivyo Watanzania bara ,wote wana haki SAWA JUU YA NCHI YAO....

Cha kushangaza tu ni wewe KUITAJA PASU KWA PASU 🤣🤣🤣

Yaani IDADI YA WAZANZIBARI walioko Zanzibar haizidi wakazi wa mkoa 1 wa bara (ndani yake pia ina wazanzibari walioko bara) halafu unaisogeza hiyo PASU KWA PASU 🤣🤣🤣🤣

Karibu gahwa akhui!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…